ZILIANZA kama tetesi, zikaja kama uvumi kuhusu ishu ya Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Mzambia Charles Haalubono kuondoka kikosini hapo na kumpisha Edna Lema ‘Mourinho’. Na sasa ishakuwa rasmi sio stori tena.
Sasa habari za uhakika ni kwamba baada ya mazungumzo ya muda mrefu hatimaye Mourinho amekubaliana na viongozi wa timu hiyo kuinoa kwa msimu ujao.
Mmoja wa viongozi wa Yanga (jina tunalo) aliliambia Mwanaspoti kuwa, Edna tayari amesaini mkataba wa mwaka mmoja.
“Tunasubiri Kocha Charles amalizie kusimamia michezo miwili iliyosalia kisha tutamtangaza Edna kuwa kocha mkuu alitoa masharti ya kutaka majukumu ya kuingia sokoni mwenyewe kusajili ili kupata wachezaji wenye ushindani,” alisema kiongozi huyo.
Edna Lema Mourinho alipotafutwa kuzungumzia juu ya usajili wake Yanga aliendelea kusisitiza kuwa “Ni kweli sina mkataba na Biashara lakini tusubiri kama ni kweli mtajua tu.”
Edna Lema “Mourinho” sio mgeni katika kikosi hicho kwani kabla ya kwenda Biashara United ya Mara iliyopo Chamspionship aliwahi kupita Yanga Princess.
Kikosi hicho cha wanawake cha Yanga kimekuwa hakina makali na hakitishi kama ilivyokuwa kipindi, kinafundishwa na Edna Lema, huku kikiwa hakina ubingwa wa Ligi hiyo.
Katika mkutano mkuu wa Yanga, Rais wa klabu hiyo Injinia Hersi alisema kwamba anaelewa kuwa Yanga Princess haifanyi vizuri zaidi kwenye ligi ya wanawake, hivyo atapambana kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri.
SOMA NA HII WAKATI PACOME IKIMBWA SANA ...AZIZ KI KWAKE NI TOFAUTI KABISA...ANAYEMKUBALI HUYU HAPA..