Habari za Simba
Habari za michezo

SIMBA TENAA…WAMKOSA MCHEZAJI MWINGINE WA MAANA KWA ‘KUJIUMA UMA KUFUNGUA POCHI’…..

admin December 16, 2022 11:02 am

Aliyekuwa Kiraka wa Klabu ya Mtibwa Sugar, Nickson Kibabage amekamilisha usajili wa kujiunga na na Klabu ya Singida Big Stars Kwa Mkataba wa Miaka mitatu kama Mchezaji huru.

Kibabage ametimkia Mkoani Singida, baada ya Uongozi wa Mtibwa Sugar kukubali kumuachia kwa makubaliano maalum na Viongozi wa Singida Big Stars, ambao wamekubali kununua sehemu ya mkataba wake iliyokuwa imesalia klabuni hapo.

Kwa mantiki hiyo Kibabage ambaye aliwahi kucheza soka nchini Morocco akiwa na Klabu ya Difaâ El Jadidi na baadae kutolewa kwa mkopo Youssoufia Berrechid, muda wowote atatangazwa ndani ya Singida Big Stars.

Kibabage mweye umri wa miaka 22 alikuwa anawaniwa pia na Miamba ya Soka ya Tanzania Simba SC lakini ofa ya Klabu hiyo ya Msimbazi ilikuwa ni kumsajili kinda huyo mwishoni Mwa Msimu Baada ya Mkataba wake na Mtibwa kumalizika.

Usiku wa kuamkia jana Kibabage aliwaaga rasmi Mashabiki wa Mtibwa Sugar kwa kuandika ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram: Nipende kutoa shukrani zangu kwenu familia yangu ya muda wote @mtibwaofficial tumeanza na wakati mzuri kwenye huu msimu nawashukuru kwa upendo mlionionesha kijana wenu naimani tutakutana wakati mwengine tena mwenyezi Mungu azidi kuwapa moyo huo huo UNITED WE STAND.

RASMI…SERIKALI YAINGILIA KATI KIPIGO CHA MWAKINYO…WAZIRI ATOA MSIMAMO HUU… ISHU YA BASI LA SIMBA KUTOONEKANA….UKWELI UKO HIVI….BARBARA ALIHUSIKA A-Z…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply