Home Habari za Yanga Leo YANGA KUTAMBULISHA KITABU CHAO LEO…ALI KAMWE ATOBOA YALIYOMO

YANGA KUTAMBULISHA KITABU CHAO LEO…ALI KAMWE ATOBOA YALIYOMO

Habari za Yanga leo

NI SIKU rasmi ya Mabingwa wa kihistoria Yanga SC kuandika historia nyingine, wanachama na mashabiki wa timu hiyo leo watashuhudia kitabu chao chenye historia mbalimbali.

Uzinduzi wa kitabu hicho ni leo Jumamosi Juni 15 ambapo uongozi wa Yanga umebainisha kwamba umekusanya mengi ya muhimu bila kuacha chochote.

Ipo wazi kwamba kwa msimu wa 2023/24 Yanga imetwaa taji la Ligi Kuu Bara, CRDB Federation Cup na ilitinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa jambo hilo la uzinduzi wa kitabu limekuwa likisubiriwa kwa shauku kubwa limefanyika kwa umakini mkubwa ili
kuwapa yale yaliyo muhimu mashabiki na wanachama.

“Ni jambo la kihistoria tunakwenda kufanya Yanga ni klabu yenye miaka 89 na kuna mengi ambayo wanachama na mashabiki wanahitaji kuyajua kazi hii tumeanza kuifanya miezi saba iliyopita na safari hii hatujaacha chochote.

“Mashabiki na Wanachama wanahitaji kupata kile kilicho bora na tunaamini kupitia hiki kitabu kuna simulizi nyingi nzuri watakutana nazo ambazo zinaeleza namna ilivyokuwa tangu awali mpaka sasa.”

Msimu uliopita klabu hiyo  Ilizindua Makala yao “Documentary” iliyoelezea matukio muhimu ya klabu ya Yanga, kitu hichi kinakuwa ni mara ya kwanza timu za hapa Tanzania kufanya hivyo, haswa upande wa kitabu, lakini   huko kwenye Makala pia klabuu ya Mtibwa Sugar ilishawahi kufanya.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF KESHO....MASTAA WAKUBWA YANGA KUKOSEKANA...NABI AANZA KULIA NA RATIBA KUBANA...