Uncategorized

SAA SABA MCHANA KESHO NDANI YA SIMBA ACHA KABISA

admin May 22, 2020 2:47 pm

INAELEZWA kuwa uongozi wa Simba umepanga kesho saa saba kutambulisha mashine mpya ya kazi ambayo itakuwa inatumika ndani ya timu hiyo ambayo ipo kwenye mkakati wa kuboresha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.


Kupitia mitandao ya kijamii, msimu huu wa 2019/20 Simba ilitambulisha mashine mpya za kazi majira ya saa saba ikiwa ni pamoja na Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael ambao walitoka Yanga, Deo Kanda, Wilker da Silver, Tairone Santos na wengine wengi jambo ambalo kesho wanataka kulizindua upya ila kwa mtindo tofauti.

Habari zinaeleza kuwa jambo litakalotambulishwa kesho ni kambabe kwa ajili ya kurahisishia kazi zao ndani na nje ya uwanja.

“Jambo kubwa linakuja na litawashangaza wengi kwani hesabu za Simba ni kuimariisha kila sekta sasa kinachotambulishwa kesho ni mtambo mpya ambao utakuwa na lengo la kurahisisha kazi, mashabiki na wapenzi wa Simba wakae mkao wa kula ni jambo jema, itakuwa live kila You Tube na Istagram na watafurahi,” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa upande wa meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa bado hajapata taarifa rasmi ya kitakachofanyika kesho hivyo hawezi kuzungumzia suala hilo.
MTIBWA SUGAR YAPOKEA TAMKO LA MAGUFULI KWA MIKONO MIWILI HIZI HAPA ZILIZOTINGA HATUA YA ROBO FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply