Uncategorized

MTIBWA SUGAR YAPOKEA TAMKO LA MAGUFULI KWA MIKONO MIWILI

admin May 22, 2020 2:47 pm


UONGOZI wa Mtibwa Sugar, umesema kuwa tamko la Rais John Magufuli wamelipokea kwa mikono miwili kwa sasa wanasubiri ratiba ili wamalize mechi zao za Ligi Kuu Bara zilizobaki.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa walikuwa wamekosa burudani kwa muda mrefu kutokana na ligi kusimamishwa kwa sababu ya maambukizi ya Virusi vya Corona.

“Machi 17 tulivunja kambi rasmi baada ya tamko la Serikali kuamua kusitisha masuala yote ya mikusanyiko isiyo ya lazima jambo lililotufanya nasi pia tutii bila shurti.

“Tamko la Magufuli ni jema na lina angalizo kuhusu afya zetu hivyo viongozi tumelipokea kwa mikono miwili na tunamwambia Magufuli asante kwa kuwa ni mwanamichezo na anapenda kufuatilia michezo kwa sasa tunasubiri ratiba tujue zinakuaje ili tuanze kujipanga kumaliza mechi zetu,” amesema.

PICHA LA LIGI KUU BARA LITACHEZWA NAMNA HII SAA SABA MCHANA KESHO NDANI YA SIMBA ACHA KABISA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply