Home Habari za usajili Bongo USAJILI WA SAIDO WAPAMBA MOTO…KUTUA TIMU MOJA KUBWA HAPA NCHINI

USAJILI WA SAIDO WAPAMBA MOTO…KUTUA TIMU MOJA KUBWA HAPA NCHINI

HABARI ZA USAJILI

SAA chache baada ya kutemwa na Simba, kiungo Saido Ntibazonkiza amepigiwa simu na moja ya vigogo wa juu wa Namungo akitaka huduma yake kwa msimu ujao.

Saido aliyemaliza msimu uliopita akiwa kinara wa mabao kwa Simba akifunga 11 na kwa sasa yupo kwao Burundi, lakini amepigiwa SIMU na kigogo wa Namungo, huku akitajwa pia Coastal Union na KMC.

Hatma  yake ndani ya Simba imedumu kwa miaka 2 tu, akitokea Geita Gold kabla ya hapo, alipita Yanga nakucheza kwa mafanikio makubwa.

Sababu moja wapo inayoelezwa kumfanya aachwe na Simba, ni umri wake kuwa mkubwa sana, hivyo Uongozi wa Simba wakaona waachane nae ili kutafuta damu changa itakayoendana na kasi ya soka la kisasa.

Ukiangalia suala  la mchango kwenye timu na takwimu zake uwanjani, bado Saidoo alikuwa na namba nzuri sana, kuliko hata baadhi ya wachezaji waliobaki kwa sasa pale Msimbazi.

SINGIDA BLACK STARS KUMEWAKA MOTO

MSHAMBULIAJI wa Singida Black Stars (zamani Ihefu), Ismail Mgunda yupo katika mazungumzo ya kujiunga na Mashujaa ya Kigoma.

Nyota huyo aliyewahi kuichezea Tanzania Prisons, awali alifuatwa na Simba waliohitaji saini yake ila kwa sasa inaelezwa hakuna mawasiliano yanayoendelea baina yao hivyo Mashujaa kuingilia dili hilo.

KMC FC KUMUONGEZA MKATABA MOALLIN.

KLABU ya KMC imeanza mazungumzo ya kumpa mkataba mpya kocha mkuu wa kikosi hicho, Abdihamid Moallin kwa ajili ya msimu ujao.

Kocha huyo wa zamani wa Azam FC, alijiunga na KMC Julai 12, 2023 akichukua nafasi ya Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na kuonyesha uwezo mkubwa jambo lililowavutia mabosi hao kutaka kuendelea naye.

SOMA NA HII  AHMED ALLY AFUNGUKA SAKATA LA AISHI MANULA KWENDA AZAM FC.