Home Habari za Simba Leo JOSHUA MUTALE ATUA DAR KIMYA KIMYA…SIMBA WAMALIZA KILA KITU

JOSHUA MUTALE ATUA DAR KIMYA KIMYA…SIMBA WAMALIZA KILA KITU

HABARI ZA SIMBA

SIMBA inaendelea kusuka kikosi chake kimyakimya huku ikielezwa kwamba kati ya mastaa 12 wa kigeni waliomaliza na kikosi hicho msimu wa 2023-2024, ni nyota watatu tu wanaobaki kwa ajili ya msimu ujao.

“Je wanaokuja wataweza kweli!” Hilo ni swali unaloweza kujiuliza kuhusiana na timu hiyo kwa msimu ujao. Katika wachezaji hao watatu wa kigeni wanaobaki anaongezwa Aubrin Kramo ambaye alijiunga na timu hiyo msimu wa 2023-2024, lakini hakucheza mechi za mashindano kutokana na kuuguza majeraha ya muda mrefu, jina lake likawekwa kando. Kwa sasa amepona na anarudi kukiwasha.

Habari njema za uhakika kabisa tulizo nazo Soka La Bongo ni kwamba mchezaji wa Zambia Joshua Mutale kama tulivyoripoti siku za nyuma, ni kweli amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka 3.

Hadi sasa tayari mchezaji huyo pamoja na familia yake wapo nchini kwaajili ya makazi, huku mchezaji huyo akisubiri taratibu zote kukamilika.

Joshua Mutale ni usajili wa tatu wa Simba wenye uhakika anaweza kucheza nafasi nyingi za ushambuliaji, kama namba 10.

Ametokea timu ya Power Dynamos ya nchini Zambia, mchezaji huyu ni miongoni mwa wachezaji wa kigeni waliosajiliwa pale Simba, wengine ni Steve Mukwala, Augustine Okejepha, Elie Mpanzu na wachezaji wengine kibao.

SOMA NA HII  KWA HILI LA YANGA, SIMBA INAPATA TABU SANA