Kocha Kijana Mohammed Mrishona Mohammed maarufu kama Kocha Xavi kutoka Tanzania ndiyo Kocha mwenye umri mdogo zaidi kwa sasa hapa Afrika mwenye leseni ya CAF A Diploma.
Mohammed Mohammed (Xavi) ni Kocha Mkuu wa Simba U20 vile vile ni Kocha wa Timu ya Vijana ya Zanzibar kuanzia U15 na U17, mwaka jana alikua Kocha Msaidizi wa Serengeti Girls (U17).
Moja ya mafanikio ya Kocha Xavi ni kuwapa Ubingwa Zanzibar katika Mashindano ya Cecafa Mwaka jana yaliyofanyika Uganda chini ya miaka 15.
Moja ya mchango wake ndani ya Simba U20 ni kuifikisha hatua ya nusu fainali msimu huu huku ikiwachukua Simba SC zaidi ya miaka 4 kufika hiyo na wakati anaichukua ilikua inaburuza mkia “wa mwisho kwenye kundi.”
Mwaka 2023 Kocha Xavi aliingia kwenye kinyanganyiro cha kuwania kocha Bora wa mwaka 2023 Tunzo za BMT ila hakufanikiwa kushinda.
Kwa sasa anafanya kazi bora sana haswa kipindi Ligi imesimama ya kuhakikisha Wachezaji wanakua timamu kwa programu maalumu huku
SOMA NA HII KUELEKEA MECHI NA DABI KESHO KUTWA..AHMED ALLY AIBUKA NA 'HOJA YA HAJA' HII KWA YANGA...