KAMA Tulivyoripoti Juni 19 mwaka huu kuwa Klabu ya Al Hilal ya Sudan imeingilia dili la Kiungo wa Asec Mimosas Serge Pokou, sasa ni rasmi mazungumzo yamekamilika na wamemtambulisha kujinga na klabu hiyo.
Al Hilal imempatia mkataba wa miaka 4 Serge Pokou ambaye alikuwa anahitajika pia na miamba ya TANZANIA Siba SC.
Vigogo hao wa Sudan wamedhamiria kufanya usajili wa maana katika dirisha hili la usajili kwa ajili ya kujiimarisha na michuano ya kimataifa msimu ujao.
Awali kila kitu kilikuwa sawa, upande wa Simba ulianza kumnyapia mchezaji huyo ambaye anachez eneo la kiungo, lakini miamba hiyo kutoka Sudan wameingilia dili hilo kimya kimya.
Inaelezwa kwamba Kocha Mkuu wa Klabu hiyo Florent Ibenge amekuwa ni mshabiki mkubwa wa mchezaji huyo, hivyo yeye ndiye anahusika zaidi kwenye kuhitaji saini ya mchezaji huyo kwa sasa.
Aliuomba Uongozi wa klabu ya Al Hilal ufanye juu chini mchezaji huyo apatikane, na wamsajili ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na hatimaye suala hilo wamelifanikisha.
Al Hilal iliwahi kutuma maombi ya kushiriki Ligi Kuu ya NBC kutokana na hali mbaya ya kiusalama nchini Sudan, vita vya wenyewe kwa wenyewe vilisababisha Ligi Kuu nchini humo kusimamishwa.
Baada ya kutuma maombi, Shirikisho la Mpira wa Miguu lilikubari ombi hilo kwa sharti la kwamba, watajumuihwa kwenye michezo ya Ligi lakini haitohesabiwa kwenye alama za msimamo, hali iliyowafanya kuona haina maana na hawatopata ushindani wanaouhitaji.