Home Habari za Simba Leo IBENGE AINGILIA DILI LA SIMBA…SERGE POKOU HUYOO AL HILAL

IBENGE AINGILIA DILI LA SIMBA…SERGE POKOU HUYOO AL HILAL

Habari za Simba leo- Serge Pokou

KLABU ya Al Hilal ya Sudan imeingilia kati dili la kiungo Serge Pokou wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast ambaye pia amekuwa akiwindwa na Simba kwa muda mrefu sasa.

Vigogo hao wamedhamiria kufanya usajili wa maana katika dirisha hili la usajili kwa ajili ya kujiimarisha na michuano ya kimataifa msimu ujao.

Awali kila kitu kilikuwa sawa, upande wa Simba ulianza kumnyapia mchezaji huyo ambaye anachez eneo la kiungo, lakini miamba hiyo kutoka Sudan wameingilia dili hilo kimya kimya.

Inaelezwa kwamba Kocha Mkuu wa Klabu hiyo Florent Ibenge amekuwa ni mshabiki mkubwa wa mchezaji huyo, hivyo yeye ndiye anahusika zaidi kwenye kuhitaji saini ya mchezaji huyo kwa sasa.

Ameuomba Uongozi wa klabu ya Al Hilal ifanye juu chini mchezaji huyo apatikane, na wamsajili ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Al Hilal iliwahi kutuma maombi ya kushiriki Ligi Kuu ya NBC kutokana na hali mbaya ya kiusalama nchini Sudan, vita vya wenyewe kwa wenyewe vilisababisha Ligi Kuu nchini humo kusimamishwa.

Baada ya kutuma maombi, Shirikisho la Mpira wa Miguu lilikubari ombi hilo kwa sharti la kwamba, watajumuihwa kwenye michezo ya Ligi lakini haitohesabiwa kwenye alama za msimamo, hali iliyowafanya kuona haina maana na hawatopata ushindani wanaouhitaji.

SOMA NA HII  MESSI "BYE BYE" ANAONDOKA PSG BURE...BARCELONA WAPIGA RADA ZAO HIZI