Home Habari za Yanga Leo DILI LA AZIZ KI YANGA LIMETIKI…ATIMKIA UFARANSA KULA BATA

DILI LA AZIZ KI YANGA LIMETIKI…ATIMKIA UFARANSA KULA BATA

Habari za Yanga leo

TAARIFA za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa kiungo raia wa Burkina Faso Stephan Aziz Ki amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kukipiga ndani ya Jangwani.

Nyota huyo amesaini mkataba huo Juni 16, mbele ya wakala wake bwana Zambro Traore na rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said.

Kwa sasa nyota huyo anaelekea mapumzikoni na atarejea klabuni hapo Kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Karibu mwezi sasa tetesi za Kiungo na mfungaji bora wa Ligi kuu ya NBC, Aziz Ki kutimka Yanga ziligonga vichwa vya habari.

Inaelezwa kwamba Aziz Ki alikuwa anataka dau kubwa la usajili, Kiasi cha Bil 1.3 za Kitanzania, na mshahara wa Mil 54 kwa Mwezi, mahitaji haya yaliwachanganya zaidi Yanga.

Uongozi wa Yanga chini ya Injinia Hersi ulijitahidi kumshawishi mchezaji huyo, aendelee kukipiga Jangwani, na kuahidi kutimiza mahitaji yake baadhi, hali iliyomfanya Stephen Aziz Ki kukubali.

Lakini hadi kufikia jana kila kitu Jumapili kilikuwa kimekamilika, na nyota huyo akamwaga wino kuendelea kukipiga Yanga hadi mwaka 2026, Juni 16.

Kauli ya Injinia Hersi ya kwamba atahakikisha anabakiza wachezaji wote muhimu kwenye kikosi hicho, imetimia na kilichobaki ni kuendelea na usajili wa wachezaji wengine.

Injinia Hersi wa takribani misimu mitatu sasa sajili zake zimekuwa  zikilipa zaidi Yanga,  tofauti na watani zao Simba.

SOMA NA HII  KOCHA YANGA ANATUMIA NDOTO KUPANGA KIKOSI...ALIOTA FARID ANAIFUNGA TP MAZEMBE