Home Habari za Usajili MBWANA SAMATTA KUMFUATA MSUVA…KUUNGANA NA RONALDO

MBWANA SAMATTA KUMFUATA MSUVA…KUUNGANA NA RONALDO

HABARI ZA USAJILI

NYOTA wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika timu ya PAOK ya Ugiriki, Mbwana Samatta ‘Popat’ inadaiwa anajiandaa kumfuata Saimon Msuva anayecheza soka nchini Saudia Arabia baada ya klabu ya Al Kholood iliyopanda Ligi Daraja la Pili nchini humo kutuma maombi ya kumtaka nahodha huyo wa Taifa Stars kwa mkopo.

Kama dili hilo litakamilika huenda Samatta akakutana na pacha anayecheza naye Taifa Stars, Msuva anayeichezea Al Najma katika ligi hiyo.

Samatta amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi ndani ya kikosi cha PAOK na mkataba alionao na Wagiriki hao unatarajiwa kutamatika Juni, mwakani.

Mbwana Samatta ni moja kati ya wachezaji wachache wa Kitanzania waliowahi kucheza soka la kulipwa Ulaya, akitanguliwa na Mzee Sunday Manara, baba mzazi wa Haji Manara.

Ana rekodi kubwa ya kuwa mwanamichezo bora wa ndani wa Afrika, tuzo hiyo alishinda akiwa na klabu ya TP Mazembe ya DR Congo ambayo nayo aliicheza kwa mafanikio makubwa sana, akifanikiwa kutwaa taji la Ligi hiyo na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pia akiwa Ulaya amefanikiwa kucheza mashindano makubwa ya vilabu, ambapo aliifunga klabu ya Liverpool, na baada ya kusajiliwa na klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza aliifunga pia klabu hiyo.

Mbwana Smatta pia ni moja kati ya mastaa wa kibongo ama wanasoka wenye utajiri   mkubwa, safari   yake ya soka  alianzia Mbagala timu ya mtaani kwake,  akapita Simba, ndipo alipopata nafasi ya kuonwa na TP  Mazembe waliofika Tanzania kuipiga na Mnyama Simba.

SOMA NA HII  BAADA YA PIRIKAPIRIKA ZA USAJALI KUPAMBA MOTO MOSES PHIRI AFUNGUKA HAYA KUHUSU KIKOSI CHA SIMBA