Habari za Yanga, Chama
Habari za Yanga Leo

MKWASA ATAJA NAMNA CHAMA ATAKAVYOMFUKIZISHA KAZI GAMONDI.

Abubakar July 4, 2024 12:17 pm

ALIYEWAHI kuwa kocha mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amezungumzia inshu ya usajili  wa Clatous Chama kwenda Yanga.

Clatous Chama amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili, ambapo mchezaji huyo alitambulishwa rasmi Jumatatu asubuhi,  na yeye binafsi aliwaaga mashabiki zake na wapenzi wa Simba kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

“Ilikuwa ni miaka 6 ya mafanikio na Simba sina budi kusema Asanetini Wanasimba” Sehemu ya maneno ya Chama.

Kocha Mkwasa hakuweza kukupesa macho na maneno pale alipokuwa anamzungumzia Chama, na baadae kufunguka kwa kusema Clatous Chama anaenda kumpa wakati mgumu Miguel Gamondi.

“Gamondi ni Kocha mkubwa na anao uzoefu wa kufanya kazi na wachezaji wakubwa,siku zote sisi makocha kwenye timu huwa kuna mchezaji huwa anakuwa kipenzi chako kwakuwa anafanya kitu cha ziada,anatumia akili zaidi hata ya maarifa ya mwalimu,na anakuwa na nidhamu,utajikuta unampenda.

“Sasa kwa Yanga wanao wachezaji wenye vipaji,na wanacheza kwenye maeneo yanayofanana,Gamondi anapaswa asioneshe mapenzi kwa mchezaji anayempe da,atengeneze mpango wa kuwatumia vizuri Aziz Ki,Pacome Zouzoua na Clatous Chama”

“iwapo kuna mmoja atakosa nafasi anaweza kumshushia mmoja kiwango kwa kukosa fitness halafu akajenga chuki kwa Kocha,na hawa Wachezaji wazuri mara nyingi ni vipenzi kwa Viongozi, anaweza kumchongea halafu Gamondi akawa wa kwanza kuondoka”Charles Boniface Mkwasa Kocha na mchezaji wa zamani wa Yanga!

HATMA YA TAIFA STARS AFCON KUJULIKANA LEO AHMED ALLY ATEMA CHECHE USAJILI WA AHOUA…KUHUSU HATMA YA JOBE AWEKA WAZI.