Home Habari za Yanga Leo MTAPATA TABU SANA…GAMONDI MPAKA 2026 PALE YANGA 

MTAPATA TABU SANA…GAMONDI MPAKA 2026 PALE YANGA 

HABARI ZA YANGA, Aziz Ki

Yanga SC imepanga kumuongezea mkataba wa miaka miwili kocha raia wa Argentina Miguel Gamondi utakaomalizika mwaka 2026.

Yanga wamefikia hatua hiyo baada ya kuridhishwa na ubora wa Kocha huyo, huku mipango ikiwa ni kuwa na mwalimu ambaye ameshazijua njia za ushindi.

Ali Kamwe alisema kuwa, mpango huo umeshakamilika na Gamondi ataongeza mkataba mpya muda mfupi Baada ya kurejea kutoka mapumzikoni.

“Gamondi mkataba wake ulikua unaisha kabla ya msimu kuanza na uongozi umeona ipo sababu ya kumpa mkataba mpya.

“Kila kitu kipo sawa na akirejea kutoka mapumzikoni atamalizia suala hilo,” alisema.

Yanga chini ya Gamondi ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana ndani ya nchi na nje ya nchi, Kimataifa.

Yanga ilifanikiwa kutetea ubingwa wao wa Ligi uu wa NBC, na kuweka rekodi ya kutwa taji hilo mara 30 tangu kuanzishwa kwa timu hiyo, pia ilitwaa Kombe la Shirikisho la CRDB kwa mara ya tatu mfululizo.

Kimataifa Yanga kwa mara ya kwanza ilifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali, huku ikukaribia kufika nusu fainali na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza Tanzania kufikia hatua hiyo, lakini ndoto zao zilikatizwa kwa kunyimwa bao la halali ambalo VAR iliamua haikuwa goli.

Yanga walicheza na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na miamba hiyo hadi dakika 180 za kucheza, zilitoshana nguvu na kwenda hatua ya mikwaju ya penati,  hali  iliyoamua hatma ya yanga kuendelea mbele.

SOMA NA HII  THIENRY MANZI BEKI AL AHLI AMUOMBA MSAMAHA DEBORAH