Home Habari za Yanga Leo GAMONDI HATAKI MCHEZO…AMPIGIA SIMU BEKI MPYA…AMPA MAELEKEZO HAYA.

GAMONDI HATAKI MCHEZO…AMPIGIA SIMU BEKI MPYA…AMPA MAELEKEZO HAYA.

HABARI ZA YANGA

KOCHA wa Yanga, Miguel Gamondi amepiga simu moja kwa beki mpya kutoka FC Lupopo Chadrack Boka na kumpa maelekezo mazito kuhusu msimu ujao ambapo Yanga inazidi kujinoa zaidi.

Boka ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili na Yanga akitokea FC Lupopo msimu ujao ataungana na kikosi hicho kipya, kwaajili ya kuanza kazi rasmi katika kambi ya mazoezi ambayo kuna uwezekano mkubwa ikafanyika nchini Afrika Kusini au Urusi lakini itategemea na sababu za kiusalama.

Kwa mujibu wa Mwanaspoti beki huyo alikiri kuwa kocha alimpigia akimkaribisha kwenye timu lakini kuna taarifa Gamondi alitaka kuzifahamu kuhusu kwake ambazo nyingine ni binafsi na baadhi zinafaa kutoa hadharani.

Alieleza kuwa, kocha huyo aliyeongeza mkataba wa mwaka mmoja na Yanga, alimuuliza zaidi kuhusu msimu wake uliopita ili kufahamu kwake ulikuwa vipi, lakini pia kumpa maelekezo kuhusu maisha mapya ambayo atakutana nayo hivi karibuni.

“Kocha amenipigia akanikaribisha kwenye timu lakini kuna taarifa alikuwa anataka kuzijua jinsi nilivyocheza msimu uliomalizika,” alisema Boka ambaye Yanga inadaiwa kumhamisha kutoka Lubumbashi kwenda Kinshasa nchini DR Congo ili kumkwepesha na hasira za mashabiki wa timu yake ambao hawajapenda kusikia akiondoka.

“Pia ameniambia anataka nikaonyeshe uwezo mkubwa ndani ya Yanga kwa upande wa beki wa kushoto, ameniambia nijiandae kwa ushindani kwani ubora wangu ndio utakaonipa nafasi kwa kuwa wapo wachezaji wazuri pia wanacheza eneo hilo.

“Akaniambia kuna msaidizi wake atanipigia kunipa programu ya mazoezi kipindi hiki ligi imemalizika na nitatakiwa kuifuata sawa sawa na kama sitafuata nitaanza kazi kwa adhabu,” alisema Boka.

Hata hivyo Boka alifunguka namna alivyojihisi kuongea na kocha huyo kwa mara ya kwanza na jinsi alivyoyapokea maelekezo hayo na kusema kuwa;

“Nimefurahia sana mazungumzo yake yamenifanya nijipange vizuri zaidi kwa kuona kuwa na kwenda kufanya kazi na timu yenye kocha mkubwa anayetaka mafanikio lakini zaidi ameniheshimu kwa kuwasiliana na mimi kwanza.”

“Hii ni kwa mara ya kwanza napata uzoefu wa aina hii, lakini imenipa picha jinsi gani kocha huyu yuko makini na hahitaji mchezaji asiye bora katika kikosi chake ndio maana ameiandalia na programu kabla sijajiunga na timu,”aliongeza mchezaji huyo.

Boka alishasaini mkataba baada tu ya ligi kumalizika na kuna uwezekano mkubwa akaungana na kikosi hicho cha Yanga, kwaajili ya maandalizi ya msimu ambako kuna uwezekano mkubwa wasishiriki michuano ya Kagame inayopigwa Dar es Salaam wiki chache zijazo.

Mchezaji huyo mwenye miaka 24 anaechezea mguu wa kushoto pia anauwezo wa kucheza kama winga, ni miongoni mwa wachezaji bora kwenye Ligi Kuu ya DR Congo.

SOMA NA HII  MASTAA WA YANGA HAWAAMBILIKI...MAYELE ACHACHAMAA...HUYO JOB SASA