Home Simba SC WATANO WA AL MERRIKH KUIKOSA SIMBA LEO KUTOKANA NA KESI YA CORONA

WATANO WA AL MERRIKH KUIKOSA SIMBA LEO KUTOKANA NA KESI YA CORONA


 IMEELEZWA kuwa wachezaji watano wa kikosi cha Al Merreikh hawatakuwa katika sehemu ya mchezo wa leo dhidi ya Simba wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Sababu kubwa ya nyota hao wa Al Merrikh iliyo kundi A pamoja na AS Vita, Al Ahly kukosa mchezo wa leo ni kukutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona.


Watatu walibainika mapema mwanzoni mwa wiki hii ambapo wapo karantini kwa sasa wakipewa huduma ili kurejea kwenye ubora wao.


Nyota wao wawili wamebainika katika vipimo vilivyofanyika leo asubuh saa nne hivyo jumla nyota watano watakosekana kwenye kikosi cha leo.
Kwenye kundi Al Merrikh bado haijakusanya pointi ikiwa imecheza jumla ya mechi mbili na kupoteza zote hivyo mchezo wa leo ikiwa itapoteza itakuwa imejiweka kwenye nafasi ya kushindwa kutinga hatua ya robo fainali.
Pia Simba itakutana na upinzani mkubwa kwa kuwa inacheza na timu ambayo haina cha kupoteza huku wao hesabu zao zikiwa ni kupata pointi tatu muhimu.
SOMA NA HII  JOHN BOCCO APEWA TUZO YA MFUNGAJI BORA BONGO