Home Habari za Simba Leo JOBE HUYOO ANASEPA…SIMBA KUMLIPA MIL 200

JOBE HUYOO ANASEPA…SIMBA KUMLIPA MIL 200

HABARI ZA USAJILI, SIMBA, YANGA

Simba imepanga kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wake Pa Omar Jobe kwaajili ya msimu ujao.

Jobe alijiunga na Simba katika dirisha dogo la Januari kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu lakini ufanisi wake haujawaridhisha.

Simba inamtoa Jobe kwa Mkopo ili kusajili mshambuliaji mwingine kwani kama itamvunjia mkataba itahitajika kumlipa zaidi ya sh200 mil.

Usajili Azam FC.

Azam ipo kwenye hatua za mwisho kuachana na aliyekuwa beki wake, Msenegal Malickou Ndoye.

Ndoye alijiunga na Azam mwaka 2022 akitokea Teungueth ya kwao Senegal na kuanza maisha ndani ya Azam Complex kwa kiwango bora lakini baadae aliandamwa na majeraha yaliyomfanya muda mwingi kukaa nje ya uwanja.Mkataba wa Ndoye unatamatika mwezi huu.

USAJILI YANGA.

KIUNGO Zawadi Mauya huenda msimu ujao akaichezea klabu ya Singida Black Stars (Zamani Ihefu), baada ya mkataba wake na Yanga kufika ukingoni.

Tayari viongozi wa Singida na Mauya wamefungua mazungumzo ya kusaini mkataba wa miaka miwili huku Yanga ikionekana kutomuhitaji tena Mauya aliyejiunga na chama hilo 2020 akitokea Kagera Sugar.

USAJILI MASHUJAA.

MASHUJAA iliyonusurika kushuka daraja, imepeleka ofa kwa Mtibwa Sugar ili kumnasa kipa Mohamed Makaka, kuongeza nguvu kikosini baada kuwepo kwa taarifa kipa Erick Johora amemaliza mkataba ndani ya timu hiyo ya Kigoma. Makaka bado ana mkataba na Mtibwa iliyoshuka daraja.

SOMA NA HII  YANGA YAKAMILISHA USAJILI HUU..."HII NI ZAWADI KWA MASHABIIKI WETU