Klabu ya Simba imefanikiwa kuinasa saini ya mlinzi wa kati, Chamou Karaboue raia wa Ivory Coast kutoka klabu ya Racing Club dā Abidjan kwa mkataba wa miaka miwili.
Kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo inaelezwa Chamou Karaboue amekubali ofa ya kusaini Simba mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza mmoja.
Chamou Karaboue ataungana na mchezaji mwenzake wa Ivory Coast Jean Ahoua ambaye msimu uliopita aliibuka mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Ivory Coast (MVP) huku akifunga mabao 12 na ametoa asisti tisa.
Chamou Karaboue amechaguliwa Kama mbadala sahihi wa Henock Inonga ambae ameuzwa FC Rabat ya Morocco.
Beki huyu mwenye umri wa miaka 24 anatajwa Kama beki bora wa ligi kuu ya Ivory coast iliyomalizika hivi karibuni .
Hadi sasa Simba inajumla ya wachezaji wa Kimataifa 16 huku baadhi yao wakitarajiwa kupewa Thank You muda wowote, ina Ayoub Lakred, Valentin Nouma, Che Malone Fondoh, Chamou Karaboue, Augustine Okejepha, Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute, Babacar Sarr, Deborah Farnandes, Joshua Mutake, Willy Essomba Onana, Par Omar Jobe, Fred Michael Koublan, Steve Mukwala, Jean Charles Ahoua, Aubin Kramo.
Pia baadhi ya wachezaji waliopewa Thank You klabuni hapo ni John Bocco, Saidoo Ntibazonkiza, Kenned Juma, Luis Miquissone, Clatous Chama, Henock Inonga Baka aliyeuzwa AS FAR RABAT ya Morocco.
Endapo Simba itaachana na wachezaji wake wa zamani wa Kimataifa kama inavyofahamika, Kanoute, Babacar Sar, Jobe, Onana na Aubin Kramo Simba itabakiza nafasi moja kukamilisha idada ya wachezaji 12 wa Kimataifa, nafasi hiyo anayopewa zaidi ni Elie Mpanzu wa AS Vita ambaye usajili wake upo karibuni kukamilika.