Home Habari za Simba Leo SIMBA YAHAMIA KWA MNIGERIA…DILI LA MPANZU NGUMU KUMEZA

SIMBA YAHAMIA KWA MNIGERIA…DILI LA MPANZU NGUMU KUMEZA

Habari za Simba- Jonathan Alukwu

UONGOZI wa Simba umeanza mazungumzo na Sporting Lagos FC ya Nigeria ili kupata saini ya winga wa kikosi hicho, Jonathan Alukwu, ikiwa itashindwa kumpata Elie Mpanzu kutoka AS Vita ya DR Congo.

Alukwu mwenye miaka 21, anaichezea FC Heartland, inaelezwa Simba wanajaribu kumshawishi ili ajiunge nao.

Dili la kumsajili winga huyo wa AS Vita lina ugumu kutoka kwenye timu,ย  ย licha ya mhezaji mwenyewe kuonesha nia ya kucheza soka nje ya DR Congo.

Rais wa AS Vita Diaby aliingilia kati usajili wa nyota huyo kwenda Simba, na kumsihi mchezaji husika kusalia klabuni hapo na atampa mara tatu ya kile kinachotolewa na Simba.

Lakini Elie Mpanzu mwenyewe inaeleza kishawaaga wachezaji wenzake, na kinachosubiriwa tu ni makubaliano kati yake na Uongozi wa timu yake.

Inaelezwa kwamba Kiongozi mmoja wa Simba alifika DR Congo kusukuma dili hilo, na kumchukua mchezaji huyo kumpelea Kinshasha kuepuka hatari ya mashabiki ambao nao hawataki aondoke

Simba hadi sasa imefanya sajili 11, huku ikianza na Joshua Mutale, Steve Mukwala, Jean Charles Ahoua, Augustine Okejepha, Abdulrazak Hamza, Valentino Mashaka, Deborah Farnandes, Valentine Nouma, Yusuph Kagoma, Chamou Karaboue, Lameck Lawi.

Na bado inaelezwa wataendelea kutambulisha vyuma vya kaz, ikiwa leo watatambulisha Mashine ya Ubaya Ubwela kwa mujibu wa Afisa Habari wa Klabu hiyo Ahmed Ally.

SOMA NA HII  HAPA SIMBA PALE YANGA, HUYU USHINDI YULE TREND SIO POA