ALIYEWAHI kuwa mlinzi wa kulia ndani ya Yanga SC, raia wa DR Congo Djuma Shabani amejiunga na klabu ya Namungo Kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Namungo wamefanikiwa kuipata Saini hiyo siku chache Baada ya taarifa ya kuwa Coastal Union walikuwa wamefikia pazuri kwenye kuisaka Saini ya Beki huyo.
Namungo ushawishi wao umekuwa bora zaidi ya Coastal Union ambao walikuwa vitani nao kuiwania saini yake kutokana na uwepo wa Kocha Mwinyi Zahera kwenye timu hiyo.
Muda wowote atawasili nchini Tanzania ili kuungana na kikosi hicho kipya tayari kwa maandalizi ya msimu mpya.
Klabu hiyo yenye makao makuu yao mkoani Lindi wameendelea kuimarisha kikosi chao kwa kusajili wachezaji wenye majina makubwa, itakumbukwa kikosi hicho kina nyota kama Beno Kakolanya, Erasto Nyoni na wengine wengi.
Wakati akiwa na Yanga Djuma Shabani alicheza kwa mafanikio makubwa akitwaa mataji mawili ya Ligi Kuu ya NBC, Mataji mawili ya Kombe la Shirikisho FA, na Mataji Mawili ya Ngao ya Jamii huku pia wakichukua kombe la Mapinduzi.
Nafasi ya Djuma Shabani Yanga ilichukuliwa na Kijana wa Ivory Coast Attohoula Yao Kuasi ambaye anacheza upande wa beki ya kulia, na amekuwa na msaada mkubwa sana Yanga.
Hadi sasa Yao Jeshi amebakia kuwa beki wa kulia bora kwa msimu ulioisha kwa upande wa Yanga.