Home Habari za Yanga Leo KWANINI PACOME HAYUPO SAUZI NA YANGA…SABABU NI HIZI

KWANINI PACOME HAYUPO SAUZI NA YANGA…SABABU NI HIZI

Habari za Yanga leo

BAADA ya sintofahamu ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua kutoongozana na kikosi cha timu hiyo kwenda Afrika Kusini, Tumezinyaka sababu ziliyomfanya asiwe sehemu ya kikosi hicho ni ishu ya pasipoti na amepewa siku tano kumaliza tatizo hilo kabla ya kuungana na wenzake Sauzi.

Awali kiungo huyo alikuwa pamoja na kikosi hicho tangu mazoezi hayo ya Pre Season kuanza, lakini juzi wakati timu uinaoondoka hakuwepo na ilishindikana kufahamika kwa mapema, hadi jana ilipoelezwa tatizo lililoomzuia asiondoke na wenzake ni pasipoti na amepewa siku tano kuanzia leo kuishughulikia.

“Sababu ya Pacome kutoondoka pamoja na wenzake ni pasipoti yake ilikuwa imejaa, hivyo inatakiwa arejee nchini kwao Ivory Coast kwaajili ya kupata kingine,” kilisema chanzo hicho kutoka Yanga na kuongeza;

“Kutokana na umuhimu wa sababu yake, uongozi umempa siku tano, ili akamilishe kila kitu, kisha ajiunge na wenzake Afrika Kusini, ambako watakaa wiki mbili na kurejea nchini kujiandaa na mambo mengine.”

Ndani ya hizo wiki mbili watakazokaa Afrika Kusini, Yanga itashiriki mashindano mawili ambayo ni Mpumalanga Cup na Toyota Cup, ikitarajiwa kuvaana ba timu za FC Augsburg ya Ujerumani na TS Galaxy kisha kumalizana na Kaizer Chiefs inayonolewa na kocha wa zamani wa klabu ya Yanga, Nasreddine Nabi.

Jeshi zima kwa asilimia 100 lipo Afrika Kusini  na leo   watacheza mchezo wao wa kwanza wa Kirafiki wa Kimataifa majira ya saa10:00 Jioni.

SOMA NA HII  SIMBA NA YANGA KUOGA MAMILIONI YA CAF