Home Habari za michezo KUHUSU KESI YA ENG HERSI NA VIONGOZI WAKE KUTAKIWA KUJIUZULU YANGA….MAPYA YAIBUKA…

KUHUSU KESI YA ENG HERSI NA VIONGOZI WAKE KUTAKIWA KUJIUZULU YANGA….MAPYA YAIBUKA…

Habari za Yanga

MKURUGENZI wa Sheria wa Yanga, Simon Patrick amesema wameomba Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu kuwapa muda na kupitia shauri la madai yanayowakabili Baraza la Wadhamini na uongozi wa klabu hiyo kuwa ni batili kikatiba.

Novemba 2022, Juma Ally na Geofrey Mwaipopo, walifungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, msingi wa madai yao ni kuwa hawalitambui Baraza la Wadhamini la Yanga kutokana na kutoitambua Katiba ya 2010 ambayo haijasajiliwa na RITA, wanadai wanachama wote sio halali hivyo viongozi wote na Wanachama wote ambao waliingia kwa mujibu wa katiba hiyo ni batili.

Akizungumza hayo makao makuu ya klabu ya Yanga, Simon amesema Juni 16, mwaka huu uongozi ulipokea taarifa kutoka mahakamani na kufanya uchunguzi na kugundua mambo mbalimbali.

Amesema baada ya wanasheria wa Yanga kufanya uchunguzi, walimegundua kuwa walalamikaji Juma na Mwaipopo waliofungua kesi wakitaka Rais wa Yanga, Hersi Said na viongozi wengine waachie ngazi, walighushi sahihi ya klabu na baraza la wadhamini inayoundwa na Mama Fatma Karume, Jabir Katundu na kushinikiza Mahakama iwape ushindi na iridhie wapewe timu na mali zote za klabu waendeshe wao.

“Watu hawa Juma Ally na Geofrey Mwaipopo waliojiita wanachama wa Yanga, imeitaka mahakama ituondoe katika Uongozi, pia walikuwa wanataka kazi zote zilizofanywa na Viongozi hawa zitambuliwe kama batili na waletewe mapato na matumizi yote.

Kesi ilianza kusikilizwa mlalamikiwa namba moja ikiwa ni Yanga, Mama Karume Mlalamikiwa namba mbili na Mzee Katundu, Abeid Mohamed aliwasilisha ushahidi au utetezi ambao ulisainiwa na klabu, akidai wote wamemteua kuwawakilisha katika mwenendo wa kesi hiyo, na Abeid alikuwa anakubali kila kitu kinacholalamikiwa akidai anawawakilisha wengine na ikapelekea Mahakama kuwapa ushindi Walalamikaji,” amesema na kuongeza ;

Mei mwaka huu, walalamikaji hao walipeleka maombi ya kukaza hukumu mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu wakiomba Mahakama iwasaidie kulitoa na kulifuta Baraza zima la Wadhamani wa Yanga na kuutoa uongozi wote wa klabu na kutaka wakabidhiwe timu na ‘asset‘ zote za klabu waendeshe wao,” amesema Simon.

Amesema baada ya wanasheria wa Yanga kufuatilia kiundani wakabaini wameghushi sahihi na pia walalamikaji hao sio wanachama wa Yanga, klabu hiyo itaiomba mahakama kuongeza muda wa kupitia shauri na kukata rufaa dhidi ya hukumu kwa kuwa muda wa kukata rufaa umeshapita.

Ameongeza kuwa klabu itaiomba Mahakama kuomba zuio ya utekelezaji wa hukumu na kuwafikia waliokuwa washtakiwa Katundu, Fatma na Mkuchika kwa Mambo manne ambayo Yanga watayafanya ikiwemoKuomba Mahakama kuongeza muda wa kupitia shauri na kukata rufaa dhidi ya hukumu kwa kuwa muda wa kukata rufaa imeshapita ilikuwa ya 2023.

“Kuandikia Mahakama kuomba zuio ya utekelezaji wa hukumu na kuwafikia waliokuwa washtakiwa Jabir Katundu, Fatma Karume na Mkuchika ili kushirikiana na uongozi kufungua kesi ya jinai kwq sababu ya kugushi sahihi za washtakiwa hao katika nyaraka zilizowasilishwa mahakamani.

Kutumia vyombo vya uchunguzi yenye kubaini watu hao wawili wanahusiana na kundi gani na kupeleka ushahidi huo katika mkutano mkuu ambao utaitwa wa dharula itayohusu ahenda moja. na uongozi kufungua kesi ya jinai kwa sababu ya kughushi sahihi zao katika nyaraka zilizowasilishwa mahakamani”, amesema Simon.

Amesisitiza kuwa uongozi utatumia vyombo vya uchunguzi kubaini watu hao wawili wanasaidiana na kundi gani, watakaowabaini watawapeleka katika mkutano mkuu wa dharula wenye ajenda hiyo pekee.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO...NABI ATOA KISINGIZIO MAPEMA....AWATUPIA LAWAMA TFF KWA 'KUMSINCHI'...