Habari za Simba- Patrick Rweyamamu
Habari za Simba Leo

PATRICK RWEYAMAMU ARUDI NDANI YA SIMBA

Abubakar July 22, 2024 3:15 pm

Klabu ya Simba imemrejesha kikosini Patrick Rweyemamu kuendelea na majukumu yake ya kuwa meneja wa timu hiyo.

Rweyemamu amerejeshwa katika majukumu hayo baada ya msimu uliopita kuondolewa kwenye nafasi hiyo na kuwa Mkuu wa Programu za Soka la Vijana klabuni hapo.

Kurejea kwake anachukua nafasi ya Mikael Igendia raia wa Kenya ambaye alikuwa Meneja wa Simba na Mkuu wa Sayansi ya Michezo. Kumbuka Igendia wakati anatambulishwa ndani ya Simba, alichukua nafasi ya Rweyemamu.

Baada ya kurejeshwa katika nafasi hiyo, Rweyemamu anatarajia kusafiri leo mchana kutoka Dar es Salaam kuelekea Ismailia nchini Misri kwa ajili ya kujiunga na kambi ya Simba iliyopo huko tangu Julai 8 mwaka huu.

Mpaka sasa bado taarifa za Michael Igendia kurejea ndani ya kikosi cha Simba, hazijulikani, kuna kila dalili za kocha huyo kuomba kuondoka klabui hapo ili kutafuta changamoto mpya.

Hiyo diyo sababu iliyowapelekea hata Simba kumrejesha Patrick Rweyamamu, kuchukua nafasi ya Mkenya huyo,  ambaye katika muda wa majukumu yake alikuwa pia akifanya kazi kwa ukaribu zaidi na TFF katika timu ya Taifa Stars.

HAJI MANARA ARUDI YANGA NA KAULI YA KUMKATAA ALI KAMWE. MANARA: MAMA YANGU SABABU YA MIMI KUTUMIKIA ADHABU