UNAAMBIWA mara baada tu ya kuingia kambini, nyota wa Simba, raia wa Ghana, Bernard Morrison, amejikuta akizua jambo jipya baada ya kugoma kuhamishwa chumba cha kulala.
Morrison alikuwa nje ya kikosi hicho tangu Februari 4, baada ya kusimamishwa na uongozi wa timu hiyo kwa makosa ya utovu wa nidhamu aliouonyesha kwa baadhi ya uongozi na benchi la ufundi.
Chanzo chetu kutoka kambi ya Simba iliyopo Ndege Beach jijini Dar es Salaam, kimesema kuwa, mara baada ya juzi Ju– matatu, Morrison kuwasili kambini, alijikuta akizua gumzo jipya mara baada ya meneja wa klabu hiyo, Patrick Rweyamamu, kutaka kumhamisha chumba alichokuwa akilala mwanzo, ambapo aligoma na kulazi– mika kurejeshwa kwenye chumba hicho.
“Ebwana eeh … nikwambie siku zote mtu mtundu huwa haji– fichi tabia kabisa, yaani pamoja na Morrison kusimamishwa kwa muda, huwezi kuamini jana (juzi) baada ya kurudi kambini tu alilizua jambo jipya baada ya kugoma kuhamishwa chumba na meneja kiasi cha kulazimika kurejeshwa alikokuwa awali.”Championi Jumatano baada ya kuelezwa hali hiyo, lilimtafuta Meneja Patrick Rweyamamu, ili aweze kuthibitisha uwepo wa hali hiyo ambapo alisema: “Ni kweli Morrison karejeshwa na uongozi na tayari aliingia mazoezi ya jana (juzi).
“Hivyo mimi kwa nafasi yangu nimempokea na kumuelekeza kinachotakiwa akiwa kambini, hivyo tupo naye na anaendelea na ratiba za kocha kama inavyotakiwa.”