Home Habari za Yanga Leo SUALA LA MANGALO KWENA YANGA LIKO HIVI…NI SUALA LA MUDA TU.

SUALA LA MANGALO KWENA YANGA LIKO HIVI…NI SUALA LA MUDA TU.

Habari za Yanga

TAARIFA kubwa leo kwenye soko la usajili inamuhusu pia Abdulmajid Mangalo aliyemaliza msimu akiwa na Singida Fountain Gate FC kutakiwa na Yanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Fountain Gate FC Kidawawa Thabitha Ili kujua ukweli wa taarifa hizo ambapo alisema, wana ofa nyingi kutoka hapa Nyumbani na nje ya Tanzania ikiwemo Mangalo.

“Naomba watu waendelee kusubiri, sisi tutatoa taarifa zote ambazo zinahusu wachezaji na klabu yetu. Mangalo anatakiwa na klabu nyingi, siyo tu Yanga,” alisema.

Yanga imepanga kufanya sajili kubwa zenye kuongeza ushindani katika klabu hiyo, hili limedhihirishwa kwa aina ya wachezaji wanaotambulishwa.

Ali Kamwe, Afisa Habari wa Yanga amebainisha kuwa haikuwa kazi rahisi kuwapata wachezaji wenye uwezo mkubwa hilo lipo wazi na linaongeza thamani ya ligi ya Tanzania.

“Msimu huu hata msiposema mawe yatazungumza kwamba Yanga tuna timu bora kwa kuwa kuna wachezaji wazuri wenye ubora na hilo linafanyika kwa sasa kuwa imara kila eneo ndani ya uwanja.

“Kila Mwanayanga anafurahi kwa sasa kwa sababu kila eneo kuna wachezaji bora na wenye uwezo mkubwa hili linatupa nguvu ya kuwa imara kwenye mashindano ambayo tutashiriki.”.

Usajili wa kwanza ndani ya Yanga ambao umeleta mtikisiko Bongo ni wa Clatous Chama ambaye ameibuka hapo bure akitokea Simba yeye ni kiungo mshambuliaji.

Saini ya Stephene Aziz Ki ambaye alitambulishwa Julai 10 kuwa bado ni Mwananchi ilizua gumzo barani Afrika kwa kuwa alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za timu mbalimbali.

Hadi sasa Yanga imewatambulisha wachezaji kadhaa akiwem Clatous Chama, Prince Dube, Chadrack Boka na Abubakar Khommeiny ambaye ni mlinda mlango, na Aziz Andabwile na Duke Abuya.

SOMA NA HII  MAGAZETI YA LEO: GARI LIMEWAKA UNYAMA MWINGI...WAARABU WAMEJUWA KAMA HAWAJUI