Habari za Yanga- Aziz Ki
Habari za Yanga Leo

AZIZ KI KINARA WA TUZO…BALAA LAKE USIPIME

admin August 2, 2024 11:26 am

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Sc, Stephanie Aziz Ki ameshinda tuzo ya mchezaji bora (MVP) wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2023/24.

Aziz Ki ametwaa tuzo nne ambazo ni tuzo ya MVP, Kiungo bora wa Ligi Kuu, mfungaji bora wa Ligi Kuu na Tuzo ya Kikosi bora cha msimu.

Pia Aziz Ki ameshinda tuzo ya kiungo bora wa Ligi Kuu bara msimu wa 2023-24 akiwashinda Kipre Junior wa Azam Fc na Feisal Salum ‘Feitoto’ wa Azam Fc.

Msimu uliopita Aziz Ki alifunga magoli 21, na kufanukiwa kumzidi mpinzani wake wa karibu zaidi Feisal Salum ambaye alifunga mabao 19.

Msimu huu Yanga imeongeza wachezaji kadhaa huenda wakafanikiwa kutwaa tuzo nyingi zaidi kwa msimu mpya utakapoanza, maingizo mapya Yanga ni Clatous Chama, Chadrack Boka, Duke Abuya, Aziz Andabwile,  Prince Dube, na Jean Baleke.

IBRAHIM BACCA ATWAA TUZO YA BEKI BORA. MO DEWJI APANGA SAFU MPYA YA MASHINDANO SIMBA