Home Habari za Yanga Leo STEPHEN AZIZ KI TAYARI ANA TUZO MKONONI

STEPHEN AZIZ KI TAYARI ANA TUZO MKONONI

Habari za Yanga leo

STEPHEN Aziz Ki katika msimu wa 2023/24 alifunga jumla ya mabao 21 katika Ligi Kuu Bara ndani ya uwanja akiwa na tuzo yake mkononi kwa sasa ambayo ni ile ya mfungaji bora.

Aziz Ki ni namba moja kwa watupiaji wa mabao ndani ya ligi alipofunga jumla ya mabao 21 kati ya 71 na alitoa pasi 8 za mabao ndani ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Rekodi zinaonyesha kuwa alifunga mabao 17 kwa mguu wa kushoto, mabao matatu kwa mguu wa kulia na pigo la kichwa ilikuwa bao moja dhidi ya Tabora United uliochezwa Uwanja wa Mkapa alipofikisha mabao 18.

Aziz Ki akiwa ndani ya 18 ni mabao 15 alifunga nje ya 18 alifunga mabao 6 ambapo kwenye mabao hayo alikuwa ni mkali wa kutupia kwa mapigo huru huku mguu wake wenye nguvu ukiwa ni ule wa kushoto.

Usiku wa Tuzo 2023/24 unatarajiwa kuwa leo Agosti Mosi 2024, Masaki ambapo tuzo zitatolewa kwa wachezaji pamoja na viongozi ikiwa ni mwanzo wa kuelekea msimu mpya wa 2024/25.

SOMA NA HII  RASMI...ASEC MIMOSAS WAKUBALI YAISHE KWA AZIZ KI...WAMUAGA KAMA SIMBA WALIVYOMUAGA MORRISON...