Home Habari za michezo RASMI…ASEC MIMOSAS WAKUBALI YAISHE KWA AZIZ KI…WAMUAGA KAMA SIMBA WALIVYOMUAGA MORRISON…

RASMI…ASEC MIMOSAS WAKUBALI YAISHE KWA AZIZ KI…WAMUAGA KAMA SIMBA WALIVYOMUAGA MORRISON…


Klabu ya ASEC Mimosas imemshukuru na kumtakia kila kila lakheri winga wao Stephan Aziz Ki kwenye majukumu yake mapya.

Kupitia ukurasa wao wa Instagram wameposti picha ya winga huyo na kuandika maneno kuashiria kuwa staa huyo amefikia mwisho wa mkataba wake na klabu hiyo.

Ki ameitumikia timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili na kuisaidia kutwaa mataji mawili kwenye Ligi Kuu ya nchini Ivory Cost.

Winga huyo ambaye tayari amemalizana na Yanga atatambulishwa na klabu hiyo muda wowote kwaajili ya kuongeza nguvu kikosi cha timu hiyo msimu ujao.

SOMA NA HII  KOCHA POLISI TANZANIA ACHEKELEA USAJILI WA METACHA MNATA