Home Habari za Yanga Leo MSHERY NA KHOMEIN WAJIPANGE SANA KWA DIARRA

MSHERY NA KHOMEIN WAJIPANGE SANA KWA DIARRA

HABARI ZA YANGA-DIARRA

WALINDA MLANGO wa Yanga, Abuutwalib Mshery na Khomein Abubakar wana kazi kubwa ya kufanya kumng’oa kipa namba moja wa timu hiyo, Djigui Diarra ambaye ana miaka mingine mitatu kuwapa ushindani huku wakiweka wazi kuwa sio namba tu wanajifunza mengi kutoka kwake.

Diarra aliyesajiliwa na Yanga Agosti 2021 akitokea Stade Malien ya nchini kwao Mali mkataba wa sasa na Yanga ulikuwa unatamatika mwisho wa msimu wa 2024/25, hivyo Kwa kusaini mkataba mpya wa miaka miwili unamuweka Diarra Jangwani mpaka msimu wa 2026/27.

Kipa huyo namba moja wa Yanga tangu ametua kikosini humo amefanikiwa kuibuka kipa bora wa msimu mara mbili mfululizo na ameisaidia timu hiyo kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu Bara mfululizo na mataji mawili ya Kombe la Shirikisho (FA) amekuwa panga pangua kikosi cha kwanza.

Kuongezwa kwake mkataba kumewaibua makipa wa timu hiyo ambao wamekiri kuwa licha ya kukosa kwao nafasi mbele ya Diarra wamekuwa wakijifunza vitu vingi kutoka kwake.

Mshery alisema Yanga ni taasisi ambayo kila mchezaji anatamani kuitumikia kuongezwa mkataba kwa Diarra kwake sio kikwazo anaamini muda ukifika atapata nafasi ya kucheza na atafanya kilicho bora kutokana na kujifunza mengi kutoka kwa msinsani wake.

“Anastahili kuongezwa mkataba ni sawa na mimi nimeongezwa kwa sababu kuna kitu wamekiona kutoka kwangu Diarra ni mchezaji mzuri kila mmoja anaona anachokifanya, kazi ni kwetu kupambana ili tuweze kupata nafasi, hilo linawezekana kwasababu mashindano ni mengi.” Alisema.

Khomein alisema ametua kwenye timu ambayo inampa changamoto ya kupambania nafasi hawezi kukaa kwa kujiamini na kusahau kama kuna nafasi ya kucheza hivyo atapambana kumuaminisha kocha kuwa anaweza kila atakapopata nafasi.

“Diarra ni mchezaji kiongozi ana mafanikio makubwa ndani ya Yanga bali na changamoto ya namba anayotupa amekuwa akitufundisha kuwa makipa wa aina kama yake sina wasiwasi naamini katika kupambana na kupata namba,” alisema.

Diarra kama atamaliza misimu mitatu hiyo ndani ya Yanga atakuwa ni kipa wa kigeni aliyecheza misimu mingi ndani ya kikosi cha Yanga kutokana na wengi kuja na kuondoka w

SOMA NA HII  AWESU ATOBOA SIRI...AELEZEA BAO LILE LA TABORA UTD