Home Habari za Yanga Leo KUNA MAXI NZENGELI MMOJA TU YANGA…SI PACOME, CHAMA WALA NANI

KUNA MAXI NZENGELI MMOJA TU YANGA…SI PACOME, CHAMA WALA NANI

HABARI ZA YANGA-NZENGELI

WATAKUJA Wote na watasifiwa sana lakini kuna huyu mwamba mmoja atabaki dunia yake, Chama amesifiwa sana, kuna Dube lakini Maxi Nzengeli anastahili pongezi na heshima pale Jangwani.

Atasifiwa Stephanie Aziz KI kwa kuongeza miaka mingine ya kusalia Jangwani na Twiga kwa kuwa alimaliza msimu uliopita akiwa kwenye kiwango bora kabisa basi matarajio ni makubwa kuekekea msimu ujao.

PACOME ZOUZOUA haachwi kuimbwa kwakuwa Wananchi ndio timu pekee iliyoifunga Al ahly kwenye kampeni za Caf champion league na mfungaji ni Professor kutoka Ivory coast.

Mtamsifia sana Jean Othos Baleke kwa kuwa hata kabla hajapandishwa kwenye page rasmi za Yanga kama usajili mpya basi wamempandisha kama mfungaji wa goli dhidi ya Augsburg kwa kuwa alitoka pale Kariakoo mitaa ya Msimbazi basi atatrend ila yupo Mwanajeshi mmoja kutoka DR Congo mitaa ya Kindu.

Maxi Mpiah Nzengeli hawezi kuwekwa kwenye debate nyingi za wapenda soka ila naamini kwenye kikosi cha Miguel Gamondi ambacho kimesajiliwa kwa gharama kubwa chini ya Muwekezaji Ghalibu Said Mohamed(GSM) Ila anaivaa kofia yenye kengele pale mitaa ya Jangwani na Twiga alipo yeye ndio Yanga ipo ukibisha karudie mechi ya Yanga dhidi ya Augsburg.

Kiwango bora kabisa kwenye mechi kubwa wakati Miguel Gamondi anamuita Chama nje bila kumsahau Aziz ki watu walijiuliza kocha anatoaje wachezaji wakubwa kwenye mchezo mkubwa lakini shughuli nzima alikabidhiwa MAXI NZENGELI na akakiongoza kikosi chake vilivyo.

Max Nzengeli ni moia kati ya wachezaji wanaoipa faida yanga kutokana na energy yake kubwa akiwa uwanjani Max anarahisisha kazi kwenye eneo analocheza hasa uwezo wake wa kuzuia na nakushambulia ndiomaana unaweza usimuone kwenye magoli au assist lakini kazi anayofanya Max Nzengeli pale Jangwani imetukuka.

SOMA NA HII  USAJILI WA SAIDO WAPAMBA MOTO...KUTUA TIMU MOJA KUBWA HAPA NCHINI