Home Habari za Simba Leo ATEBA AMTOA AYOUB SIMBA..FADLU AONGEZA MWINGINE BENCHI LA UFUNDI.

ATEBA AMTOA AYOUB SIMBA..FADLU AONGEZA MWINGINE BENCHI LA UFUNDI.

HABARI ZA SIMBA-AYOUB

Baada ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji Leonel Ateba, Uongozi wa Simba umefikia makubaliano ya kumalizana na Ayoub Lakred kwa lengo la kupisha usajili huo.

Ayoub ameitumikia Simba kwa msimu mmoja na kuifanya timu hiyo ikamaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo inaelezwa ameondolewa kwenye mfumo kutokana na kusumbuliwa na majeraha aliyoyapata kwenye maandalizi ya msimu mpya wa 2024 /25.

Chanzo cha kuaminikia kutoka ndani ya Simba kimeniambia kuwa Uongozi wa Simba umefanya uamuzi wa kumtoa Ayoub kutokana na kukosekana kwa huduma yake na tayari wamemsajili kipa mwingine.

Lakini pia Kocha Mkuu wa Simba Fadlu Davids amemjumuisha katika benchi lake la Ufundi mtaalamu wa matibabu na utimamu wa mwili pia na majeraha Durrel Butler πŸ‡ΏπŸ‡¦ kutoa Swallows

Butler atakuwa anashughulikia masuala yote ya recovery ya majeraha katika klabu ya Simba πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

SOMA NA HII  SIMBA WATAJA SEHEMU WATAKAYOFANYA PRE SEASON...USAJILI MPYA