Home Habari za Simba Leo BIASHARA YA AWESU ILIKUWA NA FAIDA…ONANA AIPA MAMILION SIMBA

BIASHARA YA AWESU ILIKUWA NA FAIDA…ONANA AIPA MAMILION SIMBA

HABARI ZA SIMBA-AWESU

WAKATI mabosi wa Simba wakisema wamefanya biashara nzuri kwa kumuuza kiungo mshambuliaji wake, Andre Willy Esomba Onana, rasmi kiungo Awesu Awesu ni mali ya Wekundu wa Msimbazi.

Juzi Simba ilitangaza rasmi imemuuza Onana kwenda klabu ya Al Hilal Benghazi ya Libya, nyota huyo alijunga kwa Wekundu wa Msimbazi msimu uliopita na kupewa mkataba wa miaka miwili.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema ‘biashara’ ya mchezaji huyo imekamilika baada ya klabu hiyo ya Libya kufikia bei waliyokuwa wakiitaka.

“Onana amejiunga na Al Hilal Benghazi ya Libya baada ya pande zote kufikia makubaliano ya biashara, klabu tunamshukuru Onana kwa muda wote aliokuwa na sisi na tunamtakia kila heri katika maisha yake mapya ya soka ndani ya klabu hiyo,” alisema Ahmed.

Onana alijizolea umaarufu baada ya kufunga magoli mawili katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi Wydad Casablanca iliyochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa msimu uliopita.

Aliongeza Simba pia imemalizana na KMC na kwa sasa rasmi kiungo, Awesu Awesu ni mali ya klabu yao.

“Uongozi wa klabu ya Simba unapenda kuujulisha Umma kuwa Simba na KMC zimefikia makubaliano hivyo mchezaji Awesu Ally Awesu ni mchezaji halali wa klabu yetu,” alisema Ahmed.

Naye Mwenyekiti wa KMC, Herry Misinga, alithibitisha mchezaji huyo kujiunga na Simba baada ya pande zote hizo mbili kufikia makubaliano.

“Ni kweli tumemalizana na Simba, wamefuata taratibu na tumeafikiana, Awesu ni mali ya Simba, sisi KMC tunamtakia kila la heri,” Misinga alisema.

SOMA NA HII  CHILUNDA APEWA MTIHANI HUU NA UONGOZI WA SIMBA