HABARI ZA YANGA-Injinia Hersi
Habari za Yanga Leo

YANGA YAJIAPIZA KUNOGESHA UZINDUZI WA CAF.

Abubakar August 23, 2024 2:03 pm

YANGA Imejipanga kushinda ushindi mkubwa zaidi kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Vital ‘O katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Mlinda mlango wa klabu hiyo AbdulTwalib Mshery alisema kwamba wachezaji wenzake na yeye wanafahamu jukumu kubwa lililopo mbele yao, na hivyo wamejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda.

“Tutafuata maelekezo ya mwalimu kama ambavyo atatuelekeza. Hatufikiri mechi iliyopita, tunatazama mchezo ujao. Mchezo unaokuja kwetu ni kama tunaanza upya bila kujali yaliyotokea.

“Tunayo hamasa kubwa kuhakikisha kuwa tunashinda mchezo unaokuja. Kiukweli tunaitamani sana hela ya Mama (Rais Samia), hivyo tunakwenda kujitolea kwa kiwango kikubwa”

“Tumeambiwa siku ya hapo kesho itakuwa siku maalumu kwa CAF. Nafahamu mashabiki wetu nasi kwa ujumla wetu tunajivunia sana kupata wasaa wa kuandaa jambo la namna hii. Sisi kama wachezaji lazima tuhakikishe tunaiheshimisha siku hii kubwa”

KUHUSU INSHU  YA MZIZE…ALLY KAMWE ATULIZA PRESHA MECHI  YA SIMBA VS FOUNTAIN GATES IPO PALE PALE