Home Habari za Yanga Leo YANGA YAWEKA REKODI NYINGINE CAF

YANGA YAWEKA REKODI NYINGINE CAF

habari za yanga leo

KLABU ya Yanga imeweka rekodi nyingine Afrika, kwa kuwa klabu ya kwanza kuandaa mkutano wa waandishi wa habari klabuni kwao.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Yanga ambayo ilitolewa na Afisa Habari wa klabu hiyo Ali Kamwe, alisema kuwa ni heshima kubwa kwao kuandaa mkutano huo.

“Tumeweka rekodi ya kwanza ya klabu kufanya mkutano mkubwa wa CAF, tunazungumzia ukumbi na sio chumba. Jambo hili ni heshima kubwa sana kwetu, kimsingi tumeheshimisha soka la Tanzania.

“Tunawaalika sana Chamazi kutakuwa na burudani kubwa sana, tutakuwa na DJ Ally B pamoja na wasanii mbalimbali ambao tutawatangaza. Kwahiyo tujitahidi kadiri iwezekanavyo tuwahi kukata tiketi mapema sana” @alikamwe

SOMA NA HII  BALEKE AANDIKA REKODI HII MOROCCO...LIGI YA MABINGWA AFRIKA