Home Habari za Yanga Leo KUHUSU INSHU YA MZIZE…ALLY KAMWE ATULIZA PRESHA

KUHUSU INSHU YA MZIZE…ALLY KAMWE ATULIZA PRESHA

HABARI ZA YANGA-CLEMENT MZIZE

BAADA ya Klabu ya Wydad Casablanca kutuma ofa yao ya pili kwenda Yanga ili kumsajili Mshambuliaji wao Clement Mzize, jambo hilo linaonekana kuwa gumu kwa klabu hiyo kumuachia.

Wydad inayonolewa na Rhulani Mukwena imetuma ofa yenye dau la Tsh Milioni 541, ambapo Yanga inasema thamani ya Mzize ni zaidi ya pesa hizo.

“Msimu huu tuna timu bora kuliko muda wowote ule, tunayo timu tishio sio tu ndani ya Tanzania hadi nje ya mipaka ya Tanzania.

“Nitashangaa kusikia watu wanasema Mzize inabidi atoke ili akakue zaidi, lakini watu hao hao hawaangalii tulipomtoa Mzize, Wananchi tupuuze maneno yao kwani lengo lao wanataka kutuvuruga. Amesema Ally Kamwe.

“Nawahakikisha Clement Mzize, bado yupo sana Yanga. Kama ndoto zenu ni Mzize aondoke kwa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu, chini ya Injinia Hersi hawezi kuondoka Yanga.

“Tunayo nguvu ya ushawishi na nguvu ya kiuchumi. Tuna wachezaji bora na watabaki kuwa bora ndani ya Yanga. Shida yenu hamuamini kama Yanga imekuwa klabu bora na kubwa AFRIKA” Ally Kamwe

SOMA NA HII  KUHUSU ENG HERSI KUVAMIA MAJUKUMU YA CEO....UKWELI USIOSEMA HUU HAPA...SENZO ALIMKIMBIA..