Home Habari za michezo MUTALE NNJE WIKI NZIMA SIMBA….FADLU AVUNJA UKIMYA UGUMU ULIOPO….

MUTALE NNJE WIKI NZIMA SIMBA….FADLU AVUNJA UKIMYA UGUMU ULIOPO….

HABARI ZA SIMBA-MUTALE

KIUNGO wa Simba, Joshua Mutale kukaa nje ya uwanja wiki moja kwa ajii ya kupona jeraha lake la nyama za paja (Hamstring Muscles).

Joshua alipata jeraha ya nyama za paja katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wa Agosti 18, 2024 dhidi ya Tabora United na kutolewa dakika ya 31 ya mchezo huo uliopigwa uwanja wa KMC , uliopo Mwenge DSM.

Akizungumza  Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema kiungo huyo atakuwa nje ya uwanja kwa siku saba akiuguza jeraha lake.

Amesema hajapata jeraha kubwa na anatarajia baada ya siku hizo akiendelea vizuri na kuwa fiti kocha Fadlu (Davids), ataangalia uwezekano wa kumtumia.

“Mechi yetu ya Jumapili, Agosti 25 , Joshua (Mutale) hayupo kwenye mipango dhidi ya Fountain Gate FC, amepewa siku saba za kupata matiabu ya jeraha lake, “ amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa baada ya siku hizo kupita jopo la madaktari wa Simba wataendelea kumchunguza na kuangalia yupo fiti asilimia 100 kwa ajili ya kucheza mechi zijazo.

Ameeleza kuwa wanakikosi kipana na kutokuwepo kwa nyota huyo mechi dhidi ya Fountain Gate FC haitawaathiri kwa sababu ya kuwepo kwa mbadala wake ambaye kocha Fadlu atamtumia.

Simba wanatarajia kushuka dimbani Jumapili Agosti 25, dhidi ya Fountain Gate FC, uwanja wa KMC , uliopo Mwenge Dar es Salaam

SOMA NA HII  GAMONDI AMEKUNA KICHWA KUHUSU KONKONI KISHA ASEMA HAYA