Wawakilishi wa Tanzania 🇹🇿 kwenye michuano ya Klabu Bingwa kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Simba Queens inashuka tena uwanjani leo kuvaana na Kenya Police Bullets katika mechi ya nusu fainali ikiwa vita ya kusaka tiketi ya kucheza Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya pili.
Kocha wa Simba Queens, Juma Mgunda alisema mchezo wa leo sio rahisi kwa upande wao kama watu wanavyofikiria kwa sababu timu zote zimejiandaa.
Katika mechi hiyo Simba itaendelea kutegemea huduma za Asha Rashid ‘Mwalala’ na Mkenya Jentrix Shikangwa wenye mabao matatu kila moja sambamba na Viviasn Corazone.