Home Habari za michezo WAKATI MECHI YA KAGERA vs YANGA IKIPANGULIWA KESHO…GAMOND ATOA NENO KWA CHAMA…

WAKATI MECHI YA KAGERA vs YANGA IKIPANGULIWA KESHO…GAMOND ATOA NENO KWA CHAMA…

Kagera vs Yanga leo

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza mabadiliko ya muda kwa michezo miwili ya Ligi Kuu ya NBC ambapo mchezo wa Kagera Sugar FC dhidi ya Yanga ambao ni mchezo namba 8, sasa utafanyika Agosti 29, 2024, saa 11:00 jioni badala ya saa 12:30 jioni kama ilivyopangwa awali.

Kwa mchezo namba tatu kati ya Namungo FC na Fountain Gate FC ambao ulipangwa kuchezwa Agosti 29, 2024 katika Uwanja wa Majaliwa, Lindi, umebadilishwa muda na sasa utafanyika saa 1:30 usiku badala ya saa 2:30 usiku.

Kwa mujibu wa TPLB, mabadiliko hayo yamefanywa kufuatia mapendekezo kutoka kwa wadhamini wenye haki ya kurusha matangazo ya televisheni, ili kuruhusu urushaji bora wa michezo hiyo.

GAMOND ATIKISA KICHWA KWA CHAMA.

Katika hatua nyingine , Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amempa tano Clatous Chama pamoja na wachezaji wengine kwa kucheza katika kiwango bora mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vital’O.

Yanga inatinga Hatua ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa jumla ya mabao 10-0 Vital’O kwa kuwa kwenye mchezo wa kwanza wakiwa ugenini ilikuwa Vital’O 0-4 Yanga na ule wa pili wakiwa nyumbani ilikuwa Yanga 6-0 Vital’O.

Chama ambaye aliibuka Yanga akitokea Simba ni mabao sita kahusika akifunga mawili na kutoa jumla ya pasi nne za mabao kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika katika mechi mbili ambazo ni dakika 180.

Gamondi amesema kuwa wachezaji wanajituma uwanjani katika kutimiza majukumu yao jambo ambalo wanastahili pongezi na mchezo dhidi ya Vital’O ule wa pili walicheza katika kiwango bora.

“Pongezi kwa wachezaji wanajituma na kufanya kazi kubwa uwanjani kwenye mchezo wetu tukiwa nyumbani dhidi ya Vital’O walicheza kwenye kiwango bora ambacho kinafurahisha na kinapaswa kuwa endelevu.”

SOMA NA HII  KWA HILI BALAA LA AZIZ KI MSIMU HUU KAZI IPO