Home Habari za Yanga Leo AUCHO AMCHAMBUA ABUYA NA KUMWAGA YA KAMBINI

AUCHO AMCHAMBUA ABUYA NA KUMWAGA YA KAMBINI

HABARI ZA YANGA

Kiungo wa Yanga Khalid Aucho ukipenda muite Daktari wa Soka, Akiwa live kwenye insta story akifanya mahojiano na Mwandishi wa Habari kutoka Kenya @bedjosessien amefunguka kuhusiana na tofauti ya Mudathiri yahya na Duke Abuya.

“Siwezi kukuambia nani ni bora baina yao ila naweza kuwatofautisha ivv… Kwanza wote ni wazuri sana wakiwa na mpira ila Duke anatumia muda kidogo kuamua afanye nini…! Mudathir ni ‘aggressive’ kuliko Duke Abuya na anapenda kuwania mpira kwa nguvu kuliko mwenzie”

“Wakati Duke Abuya amefika Yanga nilipomuona kwa mara ya kwanza sikujua anacheza nafasi gani… Alikuwa kama anapenda kushambulia zaidi ila ungemuona pembeni kama winga nikamuambia… Kama unataka kucheza mpira tulia kwenye nafasi! Kwenye mpira kama wewe ni beki cheza kama beki na sio kama straika ama vinginevyo.”

SOMA NA HII  FEI TOTO AJITABIRIA HAYA MECHI YA YANGA vs SIMBA...AMKABIDHI KAZI 'SURE BOY' MECHI YA AZAM...

1 COMMENT

  1. […] Jonas Mkude maarufu kama Nungunungu amefunguka na kusema kwamba, yeye kama mchezaji hajawahi kumroga mchezaji mwenzake Mganda Khaled Aucho. […]

Comments are closed.