Home Habari za Simba Leo SIMBA YAKIRI UGUMU WA AL AHLI…WAJIPANGA KUPAMBANA

SIMBA YAKIRI UGUMU WA AL AHLI…WAJIPANGA KUPAMBANA

Habari za Simba SC

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa wapinzani wao kwenye Kombe la Shirikisho Afrika sio wanyonge hivyo watawakabili kwa tahadhari kupata matokeo chanya kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 15 2024 nchini Libya.

Tayari Simba wameshawasili nchini Libya tangu jana Septemba 12, na maandalizi ya mchezo huo yameanza kufanyika, huku Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally kabla ya safari alizungumza haya.

“Wanasimba wanapaswa kutambua kwamba tunakwenda kucheza na Ahly Tripoli ambayo ni klabu ya pili kwa mafanikio Libya lakini ndio klabu yenye mafanikio zaidi kimataifa nchini kwao.

Mafanikio yao makubwa ni kucheza nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Afrika 2022 na robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika 2017.

“Msimu uliopita walimaliza nafasi ya tatu, Kufuatia kutoridhishwa na matokeo hayo, wakafanya usajili mkubwa ili kurejesha heshima yao.

Miongoni mwa usajili wa kushtua waliofanya ni Mabolulu ambae amesajiliwa kwa dau la bilioni 4 na inatajwa kuwa ndio usajili mkubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo

“Mechi ya kwanza ni Septemba 15, mechi hii ya ugenini tunawategemea zaidi wachezaji wetu wapambane kadri ya uwezo wao.

Mechi ya pili ni Septemba 22 Benjamin Mkapa hii inatutegemea sisi mashabiki kuipeleka Simba yetu hatua ya makundi. Tupo tayari kwa ushidani na tunaamini mchezo utakuwa na ushindani mkubwa.”

SOMA NA HII  WAKATI MASHABIKI WAKIWA 'ROHO KWATU'....FADLU KAITAZAMA SIMBA YAKE ....KISHA AKASEMA HILI..