Home Habari za Simba Leo MABULULU NI KAMA HOSSAM HASSAN TU…SIMBA WALA HAWAOGOPI

MABULULU NI KAMA HOSSAM HASSAN TU…SIMBA WALA HAWAOGOPI

habari za simba-Mabululu

2003 wakati Zamalek wanakuja Tanzania kucheza na Simba SC kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mshambuliaji aliyekuwa kwenye midomo ya watu wakati huo alikuwa Hossam Hassan mshambuliaji hatari sana kwa wakati huo.

Benchi la ufundi la Simba SC wakati huo marehemu Agrey Siang’a wakampa kazi kijana kutoka Makongo Boniface Pawasa akabaliane naye,na wakacheza kwa nafasi kama timu na kweli mpango mkakati ukalipa na mwisho wa mchezo Simba akashinda bao 1-0 bao la kichwa la Emmanuel Gabriel Mwakyusa.

Miaka 21 baadaye Simba SC wanakwenda kucheza dhidi ya Al Ahli Tripoli na mashambuliaji Mabululu ndiye ambaye yupo kwenye midomo ya watu kwa sasa.

Bila shaka watu wa ufundi wa Simba SC watakuwa wanamjua zaidi,na huwenda wakawa na mkakati mzuri wa kitimu wa kucheza dhidi ya Al Ahly Tripoli kama timu kuliko kama Mabululu.

SOMA NA HII  KWA MARA YA KWANZA...NAHODHA YANGA AFUNGUKA SIRI HII YA KUWACHAPA RIVERS