HABARI ZA SIMBA
Habari za Simba Leo

MNYAMA NA KARATA YA MWISHO LEO KIMATAIFA…AL AHLI WAINGIA UBARIDI

Abubakar September 22, 2024 9:16 am

Mnyama Simba anatupa karata muhimu leo akihitaji ushindi wa aina yoyote dhidi  ya Al Ahli Tripoli ili itinge hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mchezo huo  utapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa au kwa Lupaso majira ya saa 10:00 Jioni.

Tayari Walibya walioonyesha kuingiwa ubaridi mapema tangu walipokuja nchini kwa kuweka ulinzi wa mabaunsa na kukimbilia katika ubalozi wa nchi hiyo kama kujihami pengine kwa kile kilichofanywa na mashabiki wao wiki iliyopita kuwafanyia fujo Wekundu hao baada ya kutoka suluhu.

YANGA YATINGA MAKUNDI CAF KWA REKODI YA KIBABE…CHAMA ANAKIMBIZA TU GAMONDI ACHIMBA MKWARA…YANGA YAVUNA MABILIONI