Home Habari za Yanga Leo DILUNGA HUMWAMBII KITU KWA CHAMA.

DILUNGA HUMWAMBII KITU KWA CHAMA.

HABARI ZA YANGA-CHAMA

KIUNGO mshambuliaji wa JKT Tanzania, Hassan Dilunga amemtaja Clatous Chama kuwa ni kiungo bora aliyewahi kumshuhudia kwa miaka ya hivi karibuni kwa mastaa wa kigeni waliobahatika kucheza Ligi Kuu Bara.

Dilunga na Chama waliwahi kucheza pamoja ndani ya Simba ambapo msimu wa 2018/19 wakati timu hiyo inafuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Nkana, bao la Chama ndilo liliamua hatima yao lilipatikana kwa asisti ya Dilunga dakika ya 89.

Dilunga alisema Chama ni mchezaji ambaye amezaliwa kucheza mpira siyo kama wachezaji ambao mpira mazoezi bila kusikiliza maelekezo ya kocha wanapoteana uwanjani, lakini kwa upande wa Mwamba wa Lusaka amemtaja kuwa ni mchezaji ambaye kiwango chake ni kilekile hakishuki.

“Kwa upande wa wachezaji wa kigeni ambao nimepata nafasi ya kucheza nao Chama ni mmoja tu hakuna mwingine ananikosha aina ya uchezaji wake anaufanya mchezo wa soka uonekane ni rahisi hii ni kutokana na namna anavyocheza,” alisema.

“Nimecheza naye pamoja nimemshuhudia akiwa bora na sasa namuangalia bado naona ni yuleyule suala la kukaa nje ya uwanja akiwa na kikosi cha Yanga haina maana kwamba kiwango chake kimeshuka na ndio maana akipata nafasi anafanya kazi yake kwa usahihi.”

Dilunga alisema Chama ana kipaji kikubwa anauwezo mzuri wa kutoa pasi za mwisho lakini pia anaweza kufunga hivyo anamuofa kocha vitu viwili uwanjani kwa usahihi asipofunga pasi atatoa fasi nzuri ya mwisho.

“Ni mzuri kufunga na anajicho la kuona usahihi wa mtu wa kumpa pasi na ikamfikia kwa usahihi, unaweza kuona ni pasi mbaya lakini ikifika kwa mpokeaji inafika kwa usahihi pia anaweza kujiweka maeneo sahihi ya kufunga akiwa ndani ya boksi kukosa ni nadra,” alisema.

Kiungo huyo ambaye kwa sasa anakipiga JKT Tanzania alisema amekuwa akijifunza mambo mengi kutoka kwa Chama na wamekuwa wakizungumza mara kwa mara pamoja na kwamba hawachezi timu moja, na mazungumzo yao ni masuala ya mpira kila mmoja akimshauri mwenzake nini afanye ili kuendelea kuwa bora.

Chama kwa sasa anashikilia rekodi ya kupachika mabao mengi kwenye michuano ya kimataifa kwa wachezaji wanaocheza hadi sasa michuano hiyo akimuacha Mtanzania, Mbwana Samata ambaye ametupia mabao 20 huku yeye akifunga bao la 21 dhidi ya CBE na kuisaidia Yanga kutika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

SOMA NA HII  AZIZ KI KINARA WA TUZO...BALAA LAKE USIPIME