Home Habari za Yanga Leo NAMBA ZA CHAMA CAF ZA MOTO

NAMBA ZA CHAMA CAF ZA MOTO

Chama Yanga

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Clatous Chama amehusika kwenye mabao manane kati ya 17 yaliyofungwa na Yanga ikitinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akimfunika Stephane Aziz Ki ambaye amehusika kwenye mabao matano akifunga manne na asisti moja.

Yanga ilianzia hatua za awali kwenye michuano hiyo imecheza mechi nne na kati ya hizo imefunga mabao 17 ikianza kuitandika Vital’O mabao 4-0 ugenini, 6-0 nyumbani pia waliichapa CBE ugenini bao 1-0 ilhali nyumbani ni 6-0.

Kiungo huyo mshambuliaji kwenye idadi hiyo ya mabao manane aliyohusika nayo amefunga matatu na kutoa asisti tano.

Chama kwenye ushindi wa mabao sita ya kwanza dhidi ya Vital O alifunga bao moja na kutoa pasi zilizozaa mabao nne, hivyo alihusika kwenye mabao matano, ambapo mengine yalifungwa na Pacome Zouzoua, Clement Mzize, Prince Dube, Stephane Aziz Ki na Mudathir Yahya.

Mchezo uliofuata Yanga wakiibuka na ushjindi wa mabao 4-0, Chama alitupia kambani bao moja ambalo lilikuwa la mpira wa kutenga ambao aliukwamisha moja kwa moja kambani.

Mabao mengine kwenye mchezo huo yalifungwa na Dube, Mzize na Aziz Ki na kutinga hatua ya pili wakikutana na CBE ya Ethiopia.

Kwenye mchezo wa mkondo wa pili mchezo wa kwanza ugenini waliibuka na ushindi wa bao moja lililofungwa na Dube akiunganisha pasi iliyochongwa na Zouzoua na mchezo wa pili nyumbani walishinda mabao sita.

Mabao kwenye mchezo huo yaligungwa na Chama ambaye alikuwa mchezaji wa kwanza kufumania nyavu akichongewa pasi na Mudathir, Mzize, Duke Abuya akiunganisha mpira uliochongwa na Aziz Ki, Mudathir pasi alipokea kutoka kwa Dube, Aziz Ki, Mzize ambaye alipasiwa na Mudathir na bao la sita lilipachikwa kimyani na Aziz Ki likiwa ni bao lake la pili kwenye mchezo huo pasi kutoka kwa Chadrack Boka.

MSIKIE GAMONDI

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi alisema ana furaha kuona wachezaji wake wanaendelea kubadilika eneo la ushambuiliaji ambapo na kwamba timu yake anatamani kuiona inatumia nafasi na kumiliki mpira.

“Timu yangu imekamilika hasa eneo la ulinzi shida ni eneo la ushambuliaji ambalo muda mwingine linapwaya kutokana na wachezaji kushindwa kutumia nafasi na wakati mwingine ndio kama hivi tumeweza kutinga hatua ya makundi tukiwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga,” alisema na kuongeza:

“Ubora wa timu ni kufunga na kuto kuruhusu mpinzani kufika eneo lako hiki kimefanyika Yanga hadi tunatinga hatua ya makundi hatujaruhusu bao na tumefunga mabao mengi hili likiendelea hivi tutakuwa na wakati mzuri wa kufikia malengo.”

Gamondi alisema amewaambia wachezaji wake kila atakayepata nafasi anatakiwa kufunga mabao na hakuna mchezaji maalumu wa kufanya hivyo na ndiyo maana kila mmoja bila kujali anacheza nafasi gani amekuwa akifanya hivyo.

SOMA NA HII  SIMBA PUNGUZENI PRESHA...MSIMU HUU TIMU MNAYO