Home Habari za michezo BAADA YA KUWAADHIBU SIMBA JUZI….HII HAPA ‘SAPRAIZI’ YA USAJILI MPYA YANGA…

BAADA YA KUWAADHIBU SIMBA JUZI….HII HAPA ‘SAPRAIZI’ YA USAJILI MPYA YANGA…

Habari za Yanga leo

KATIKA kuimarisha kikosi cha Yanga, uongozi wa klabu hiyo umeweka wazi kwamba wameshusha kifaa kipya kutoka nje kwa ajili ya dirisha dogo la usajili.

Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa hivi karibuni Rais wa klabu hiyo, Eng. Hersi Said aliweka wazi kuwa atashusha nyota wapya wawili katika dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa baadaye mwaka huu.

Licha ya Kamwe kutoweka wazi jina na nafasi ya nyota huyo, imeelezwa kuwa Yanga wamemleta kiungo Charve Onoya kiungo kutoka klabu ya As Maniema ya DR Congo.

Kiungo huyo alitakiwa kujiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu, lakini dili lilifeli na safari hii mabosi wa klabu hiyo wamerejea kwa nguvu zote kumleta nyota huyo ambaye inadaiwa yupo hapa nchini.

Amesema miongoni mwa nyota hao wawili, mmoja ametua nchini Jumamosi Oktoba 19, akiambatana na kipa wao, Djigui Diarra ambaye alikuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa na kuwasili nchino na nyota huyo mpya.

“Huyo mchezaji aliyemsema Rais Hersi tumemleta alikuwepo uwanjani katika mchezo wa Kariakoo Derby na amekuja kufanya mazungumzo na kusajili tayari kwa kuanza kazi katika michuano ya kimataifa,” amesema Kamwe ambaye hakutaja jina wala nafasi anayocheza mchezaji huyo.

Amesema licha ya kikosi cha Yanga kuonekana ni ’tishio’, lakini wanaona hakijakamilika katika kiwango wanachohitaji kifike, bado wanataka kuona Yanga iliyokuwa bora na imara.

“Nataka niwaambie tu, Yanga hii bado, Januari kutakuwa na ongezeko la mchezaji mwingine wa kigeni. Kwa hiyo haijakamilika, tunahitaji kuchukuwa ubingwa wa Afrika,” amesema Kamwe.

Amesema lengo ya Yanga kwa sasa ni kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na si vinginevyo, wamezoea kuingia makumdi sasa wanasaka robo fainali.

Katika hatua nyingine Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amewapongeza wachezaji wake, kipindi cha kwanza walicheza kimkakati wakijua Simba wataingia kwa kasi.

“Nampongeza kocha wa Simba Fadlu Davids amebadilisha timu kwa kiasi kikubwa. Ubingwa safari bado ndefu na tunatakiwa kupambana katika michezo ijayo,” amesema Gamondi.

SOMA NA HII  AHMED ALLY : KAGERA SUGAR LAZIMA WAPITIE MACHUNGU TULIYOKUTANA NAYO KWAO KAITABA...