Michezo leo
Habari za michezo

CAF WAIPELEKA ‘DABI’ YA KARIAKOO KWENYE TUZO ZAO…., SHUGHULI PEVU IKO HAPA….

admin October 29, 2024 7:55 am

VIGOGO wa soka nchini, Simba na Yanga wameingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya Klabu Bora ya Mwaka Afrika baada ya kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Watani hao wa hadi wanachuana na Al Ahly na Zamalek, zote za Mısri, Petro Atletico ya Angola, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Dreams FC ya Ghana, RS Berkane ya Morocco, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Esperance ya Tunisia.

Wakati Simba ilitolewa na Al Ahly ya Mısri kwa jumla ya mabao 3-0, ikifungwa 1-0 nyumbani na 2-0 ugenini – Yanga ilitolewa na Mamelodi Sundwons kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya jumla ya 0-0.

Al Ahly ndio walioibuka mabingwa baada ya kuichapa Esperance 1-0 ugenini na sare ya 0-0 nyumbani.

Katika Nusu Fainali Al Ahly iliitoa Mazembe ikiichapa 2-0 Cairo baada ya sare ya 0-0 Lubumbashi na Esperance iliitoa Mamelodi kwa jumla ya mabao 2-0 ikishinda 1-0 nyumbani na ugenini.

Kwa Yanga huu ni mwaka wa pili mfululizo wanawania Tuzo hiyo ambayo mwaka jana ilichukuliwa na Al Ahly.

WAKATI MASHABIKI WAKITAKA MAKUBWA CAF….MIPANGO YA FADLU NA SIMBA HII HAPA… HIZI HAPA SHERIA 17 ZA SOKA UNAZOPASWA KUJUA ILI WAAMUZI WASIKUBABAISHE….