Habari za michezo
WATU WA YANGA MNAJUA HILI LA PACOME….? SIMBA, AZAM ZINANGOJA SIKU TU…
TAARIFA kutoka ndani ya Yanga zinasema bado wanaendelea kupambania namna ya kuongeza mikataba ya nyota wake wawili, Pacome Zouzoua na beki Kouassi Yao.
Kwa Yao mambo yanaelezwa ni mepesi na huenda akawa wa kwanza kusaini mkataba, huku Pacome akiendelea kusikilizia kwani ndiye mchezaji ambaye tayari ana ofa tatu mezani kutoka ndani na nje ya Tanzania.