Home Habari za michezo BEKI SIMBA AITWA TIMU YA TAIFA BURKINA FASO…..AZIZI KI AACHWA KWENYE MATAA…

BEKI SIMBA AITWA TIMU YA TAIFA BURKINA FASO…..AZIZI KI AACHWA KWENYE MATAA…

Habari za Michezo

Beki wa kushoto wa Simba, Valentin Nouma amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Burkina Faso (The Stallions), kinachojiandaa kucheza michezo miwili ya kufuzu AFCON 2025, huku nyota wa Yanga Stephane Aziz KI akiachwa tofauti na ilivyo zoeleka.

Burkina Faso itacheza dhidi ya Senegal Novemba 14, kwenye Uwanja wa Stade du 26 Mars na Novemba 14 ikiwa ugenini itacheza dhidi ya Malawi kwenye Uwanja wa Bingu.

Katika kundi L la kufuzu Afcon 2025, Burkinafaso ndiyo inayoongoza kundi ikiwa na pointi 10 sawa na Senegal inayoshika nafasi ya pili, zikitofautiana idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa, huku namba tatu ni Burundi yenye pointi tatu na Malawi ikishika mkia ikiwa haijapata pointi katika mechi nne ilizocheza.

Hata hivyo tayari Burkinafaso na Senegal tayari zimeshafuzu AFCON 2025, zitakazofanyika Morocco.

Kikosi kilichoitwa na Kocha Brama Traore

MAKIPA

Herve Koffi, Farid Ouedraogo na Kilian NIKIEMA

MABEKI

Issa KABORE, Steeve YAGO, Edmond TAPSOBA, Nasser DJIGA, Valentin NOUMA, Mohamed OUEDRAOGO, Issouf DAYO na Trova BONI

VIUNGO

Sacha BANSE, Cedric BADOLO, Saidou SIMPORE, Blati TOURE, Dramane SALOU, Kader OUATTARA, Ousseni BOUDA na Gustavo SANGARE

WASHAMBULIAJI

Ousmane CAMARA, Bertrand TRAORE, Hassane BANDE, Dango OUATTARA, Franck Lassina TRAORE na Mohamed KONAT

SOMA NA HII  BENCHIKHA AWATULIZA WANASIMBA LICHA YA USHINDI AJA NA KAULI HII