Home Habari za michezo SIMBA, YANGA ZAPEWA ‘MTELEZO’ KOMBE LA SHIRIKISHO….

SIMBA, YANGA ZAPEWA ‘MTELEZO’ KOMBE LA SHIRIKISHO….

HABARI ZA SIMBA NA YANGA

Mabingwa watetezi wa Kombe la FA, Yanga SC, wataanza safari yao ya kutetea taji kwa kucheza dhidi ya Copco FC kutoka Mwanza, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (First League). Kwa upande wa Simba SC, wao wamepangwa kuvaana na Kilimanjaro Wonders katika hatua ya 64 bora ya michuano hiyo.

Michezo hiyo inatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi ujao, ambapo timu zote mbili, Yanga na Simba, zimepangiwa wapinzani kutoka madaraja ya chini, hali ambayo pia inaonekana kwa klabu nyingine za Ligi Kuu Bara.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Yanga kukutana na Copco FC, hali sawa na Simba kukutana na Kilimanjaro Wonders. Singida Black Stars, chini ya kocha Patrick Aussems, watacheza dhidi ya Magnet FC, wakati Azam FC watachuana na Iringa SC.

Akiongelea droo hiyo ambayo ilisimamiwa na Meneja Mashindano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto, nyota wa zamani wa Simba na Yanga Danny Mrwanda alisema anaamini hii ni fursa kwa timu za madaraja ya chini kujipima ubavu wa kumudu kukabiliana na timu za madaraja ya juu.

“Zipo timu za madaraja ya chini ambazo hupambana na kufika mbali katika michuano ya FA, binafsi huwa nachukulia mashindano haya kama nafasi yao ya kujipima kabla ya kufika madaraja ya juu, inasaidia kuona kwa namna gani mnatakiwa kuongeza nguvu,” alisema nyota huyo.

Kwa upande wake, kocha wa Singida Black Stars,Aussems alisema,”Ni droo nzuri kwa upande wangu, kilichopo kwanza ni kucheza hatua kwa hatua michezo iliyopo mbele yetu kwenye ligi kabla ya mchezo huo, itakuwa nafasi nyingine kwetu.”

RATIBA KAMILI

Singida Black Stars vs Magnet FC

Kengold FC vs Mambali FC

Mashujaa VS Tukuyu Stars

Simba vs Kilimanjaro Wonders

KMC vs Black SiX

Yanga vs Copco FC

Pamba Jiji vs Moro Kids

Tanzania Prisons v Tandika United

Fountain Gate vs Mweta Sports

Azam FC vs Iringa SC

Coastal Union vs Tanesco

Tabora United vs Foysa Academy

Kagera Sugar vs Rhino Ranges

Dodoma Jiji vs Leo Tena

JKT Tanzania vs Igunga United

Mbeya City vs Mapinduzi FC

Green Warriors vs Hausung FC

Geita Gold vs Ruvu Shooting

Mbuni FC vs Giraffe Academy

Bigman FC vs Soccer City

Cosmopolitan vs Nyota Academy

Polisi Tanzania vs Bukombe Combine

African Sports vs Town Stars

Transit Camp vs Gunners FC

Mbeya Kwanza vs Mabao FC

Biashara United vs TRA FC

Stand United vs Bon Bosco

Kiluvya FC vs African Lyon

TMA Stars vs Leopards FC

Mtibwa Sugar vs Greenland FC

Songea United vs Kiduli FC

SOMA NA HII  TRY AGAIN:- NAONDOKA LAKINI KUNAWASALITI BADO....NIMEONGEA NA MO DEWJI MARA 10....