Habari za michezo
BAADA YA KUFIKA ALGERIA….MASTAA SIMBA WAANZA ‘KISINGIZIO’ CHA BARIDI KALI πππ…
Baada ya kuwasili salama nchini Algeria mlinzi wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe amesema wachezaji wapo tayari kufuata maelekezo ya walimu kwenye mazoezi ili kufanya vizuri katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Constantine siku ya Jumapili.
Kapombe amesema siku mbili za mazoezi ambazo watazipata watazitumia vizuri kuhakikisha wanapata matokeo chanya ugenini.
Akizungumza kuhusu hali ya hewa ya Algeria, Kapombe amesema ni baridi kali lakini siku zilizobaki kabla ya mchezo zitasaidia kuwafanya kuzoea mazingira.
βHali ya hewa ni baridi kali lakini tuna siku mbili za kufanya mazoezi pamoja na kuzoea mazingira tunaamini hadi kufika siku ya mchezo tutakuwa tumeshazoea,β amesema Kapombe.